Wizara ya Ardhi Ondoeni Kero hii Mapokezi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizara ya Ardhi Ondoeni Kero hii Mapokezi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Anold, Jul 28, 2011.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,378
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Mara kadhaa nimekuwa nikifika wizara ya Ardhi ili kupata huduma mbalimbali. Kero kubwa ipo sehemu ya mapokezi ambapo amewekwa mtu mmoja ambaye hukuuliza jina na sehemu unayokwenda. Hilo ni suala la utaratibu ila kwa ofisi ambayo hutembelewa na idadi kubwa ya watu kama Wizara ya ardhi nafikiri utaratibu ulioko mapokezi si mzuri kwani kuweka mtu mmoja ambaye hulazimika kuandika jina la mgeni na sehemu anayokwenda kwa kuingiza data hizo kwenye Computer hufanya eneo hilo mara kadhaa liwe na foleni kubwa bila sababu za msingi.

  Kama ingekuwa lengo ni kutaka kuhakikisha kuwa watu wasio na kazi maalum hawaingii ndani, nafikiri pangeongezwa wahudumu ili pamoja na mambo mengine wajue basi uhakika wa wageni wanaoingiia. sasa hivi pamoja na utaratibu huo wa kupanga foleni lakini ninahakika wengi hudanganya majina au eneo analokwenda hivyo kufanya utaratibu huo uwe wa kupoteza muda. Ningeshukuru wahusika kama wataliona hili na kurekebisha kasoro hii.
   
Loading...