Wizara ya ardhi imeoza kiasi hiki?

JAYJAY

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2008
Messages
2,720
Likes
993
Points
280

JAYJAY

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2008
2,720 993 280
leo asubuhi nilikuwa naangalia habari ya channel10 kuhusu kusakwa kwa matapeli watatu wa viwanja, kamanda Kova alisema kwamba hawa jamaa wanauwezo wa kutengeneza hati bandia ambayo ina taarifa sahihi kama ile halisi iliyopo wizarani.mwanzoni hii habari nilipoiskia tbc hawakueleza kwa urefu jinsi watu wanavyoweza kutapeliwa na hawa jamaa kiasi kwamba nikawalaumu wanaotapeliwa kwa uzembe wa kushindwa hata kufika wizarani kuulizia uhalisi wa hati hizo.lakini sasa nimegungua kuwa hata mimi ningeweza kuwa mwathirika.hii inaonesha jinsi gani hii wizara ilivyooza, yaani lazima kutakuwa na mfanyakazi au wafanyakazi wanaoshirikiana na matapeli hao.kazi kwelikweli inabidi ifanyike kuisafisha hii wizara, ndio maana migogoro ya viwanja haiishi.hawa jamaa sasa wanasakwa na kifuta jasho cha shilingi milioni tano kimeahidiwa na kamanda Kova, hapo nadhani ni baada ya kigogo mmoja kupigwa hela nyingi ndio wanashtuka sasa maana siku zote hizi kilele zimekuwepo na hakuna aliyejali. tuombe wadakwe, labda mengi yatajulikana.
 

Marigwe

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Messages
226
Likes
4
Points
33

Marigwe

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2009
226 4 33
Na mimi nilimsikia Kova. Maelezo yake yameficha kitu. Hakuwa elaborate hata kidogo. Iweje hao matapeli wagushi bila ya kushirikiana na Kamishna wa Ardhi pale Wizarani? Au Katibu Mkuu au Registrar wa Ardhi. Mimi ningekuwa yeye nisingeitoa taarifa ile kama lengo si kusema kila kitu.
 

MaxShimba

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2008
Messages
35,816
Likes
132
Points
160

MaxShimba

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2008
35,816 132 160
Kwanini Serikali isiweke historia ya ardhi kwenye mtandao. First world kuna vitengo maalumu vinavyo husiana na ardhi na utapata habari ya kiwanja na/au nyumba na/au condominium, etc chechote kile kwa hadi miaka 100 iliyo pita. Kwa mfano, deeds ziwekwe online na waweke chain of title, ili mtu asisema ardhi fulani ni kiwanja chake wakati public information zinaonyesha mwenye kiwanja ni mtu mwingine. If there is a mortgage kwenye kiwanja, au dispute fulani, ziwe zinarekodiwa na kuwa public information.

Huu ujima wa akili Tanzania utaisha lini? Kiongozi wa nchi anachaguliwa halafu anacho fanya ni kufungua mafaili tu na wala hana mawazo yakinifu ya kujenga nchi. Hawa viongozi wana udhi sana.
 

Forum statistics

Threads 1,191,647
Members 451,726
Posts 27,716,446