KIDODI ONE
Member
- Apr 15, 2015
- 19
- 14
Habarini wanajukwaa.
Kituo hiki cha afya kipo wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro,kilomita chache kutoka kiwanda cha sukari.
Kuna taarifa za mama wajawazito kupoteza maisha mara kwa mara kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni uzembe wa wakunga.
Kuna mama mjamzito alipoteza maisha mwishoni mwa mwezi wa January,taarifa kutoka kwa ndugu zake zinasema kuwa marehemu ulikuwa ni uzao wake wa tatu,alipimwa akaonekana kuwa mtoto ametanguliza matako, lakini manesi wa hapo wakalazimisha kumzalishia hapo kituoni badala ya kupelekwa hospitali kibwa na matokeo yake yule mama alipoteza damu nyingi na kufariki dunia akaacha kichanga.
Kuna taarifa kuwa juzi tarehe 05.02.2017 kuna mama mwingine amepoteza maisha na kichanga chake wakati wa kujifungua.
Taarifa zinasema kuwa mjamzito alikosa msaada wakati wa kujifungua ilhali manesi walikuwepo. Watu wa karibu wanasema marehemu aliita kuomba msaada lakini hakuna nesi aliyejitokeza,mpaka wanakuja mambo yalishaharibika hatimaye wakampoteza ndugu yao na mwanaye.
Hawa waliopoteza maisha kwa uzembe sio ndugu zangu kwa nasaba,ni Watanzania wenzangu, na kituo hiki cha afya kinalalamikiwa sana kwa huduma mbovu hasa kutowajali wagonjwa. Wananchi wanaopatia huduma kituoni hapo wanalalamikia tabia ya wahudumu kuwa busy na simu zao kuliko wagonjwa.
Hiki kinachosemwa kuwa ni uzembe kisipodhibitiwa huenda kesho na keshokutwa madhara yakaongezeka na kuendelea kuwapoteza ndugu zetu.
Naomba wahusika wafuatilie hiki kituo cha afya kwa manufaa ya watanzania wenzetu wanaotegemea kituo hicho kupata huduma za kiafya.