Wizara 3 zaungana kuwasaka wazushi wa ajira za Waalimu

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Makatibu wakuu wa wizara za Mawasilino, Elimu na TAMISEMI nchini Tanzania wamezitaka mamlaka husika ikiwemo ya jeshi la polisi kumbaini mtu aliyesambaza taarifa walizodai ni za upotoshaji zinazosema kuwa ajira za ualimu kwa mwaka 2015-2016 zimesitishwa.

Wakizungumza kwa pamoja leo jijini Dar es salaam makatibu hao wamesema taarifa hizo zilizopo kwenye mitandao ya kijamii zina lenga kuleta chuki baina walimu hao na serikali, jambo ambalo ni lazima wahusika watafutwe na kuchukuliwa hatua.

Akizungumza katika mkutano huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Faustini Kamuzora amesema wizara yake imeanza kulifanyia kazi suala hilo na itahakikisha aliyehusika kusambaza taarifa hizo za uongo anabainika na kuchukuliwa hatua.

Amesema sheria ya makosa ya mitandao ndiyo itatumika katika kumtafuta na kumkamata huku akisisitiza kwa watumiaji wa mitandao kuitumia teknolojia hiyo kwa malengo mazuri na sio vinginevyo.

Chanzo: EATV
 
Wasitafute mchawi wakati ni wao wenyewe wanatoa kupima Munkari za wahusika wanaotegemea kuajiliwa zikoje
 
Kweli aisee madhara aliyo sababisha huyo mtuni makubwa sana hasa kwa walengwa ,
 
Umoja wa vyama vya upinzani unaitwa UKAWA, hawa umoja wa wizara zao unaitwaje!!? nauliza tu.
 
Nafikiri wangeweka mambo wazi kwamba ni lini ajira za hao walimu zitatoka, ili kumaliza mzizi wa fitina, kuliko kuhangaika kumtafuta huyu mzushi wa habari. Maana hawa wazushi lengo lao ni kuichokoza serikali kujua kama ni lini wanaajiri waalimu wapya.
 
Wizara zifanye mambo ya maana, sio kushughulika na mambo madogo madogo kama haya ya mitandaoni.

Madawati ya kutosha watoto kukaa washapata??
Madogo madogo mwisho huwa makubwa kweli kweli. Lazima wayatatue mapema
 
Wizara zifanye mambo ya maana, sio kushughulika na mambo madogo madogo kama haya ya mitandaoni.

Madawati ya kutosha watoto kukaa washapata??
Mkuu wewe unaliona dogo? Kweli tuna uelewa tofauti, unajua taharuki waliyowapa wahitimu wanaosubiri ajira?

Lakini pia, jamii yenye watu waongo na wazushi wanaotaka kuchonganisha serekali na watu wake ni jamii iliyokosa maadili.
 
Back
Top Bottom