mult_talented_p
Senior Member
- Oct 10, 2016
- 103
- 120
Mimi ni mwanafunzi wa shahada ya kwanza katika chuo kikuu cha Ruaha. Na pia ni mdau wa maendeleo ya elimu nchini, hususan elimu ya juu.
Tukijua ya kwamba, wanachuo wengi ni vijana ambao wameaminiwa na jamii kuwezesha kufikia ndoto zetu za maendeleo kama nchi ya Tanzania, nawasihi vijana na wanafunzi wa elimu ya juu kote nchini, tutumie nafasi zetu vizuri kwa ajili ya kukwamua nchi yetu kutoka kwenye hali iliyopo sasa na kufanikisha mapinduzi ya kiuchumi, kitamaduni, kisiasa na hata kiroho.
Tukiwa chuoni, hatuna budi kutumia akili zetu, vipawa vyetu pamoja na, mitandao yetu (social connections) kwa viwango vya hali ya juu.
Tukuze majina ya vyuo vyetu kwa maendeleo ya kielimu, na kuwa wabunifu, tukiacha alama vyuoni na hata katika jamii inayotuzunguka.
Natoa rai kwa wakufunzi wetu, na wasimamizi wetu tukiwa chuoni kuwa, wazidi kushirikiana na wanafunzi katika shughuli za kitaaluma na za kijamii. Ushirikiano huu ukidumu, utatuunganisha wote katika safari ya kufikia nchi iliyoendelea.
Kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu, nawasihi watakapoanza masomo, wajipange kufanya vitu vya tofauti, vya kufanya walimu na jumuiya yote ya vyuo, kujivunia, kwa kuja kwao.
Mwisho kabisa napenda kuwakaribisha chuo chetu cha Ruaha Catholic University, mojawapo wa visiwa vya elimu na maendeleo ya jamii, Tanzania.
Ahsante.