VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Wakati fulani,mwaka huu,nilikuwa Zanzibar. Nikapata nafasi ya kujionea yanayoendelea na kuzungumziwa kule kuhusu uchaguzi uliofutwa wa mwaka jana. Nikawa Unguja na Pemba. Kote.
Nilisema humu,nilipokuwa kule,kuwa Wazanzibari hasa wa Kisiwa cha Pemba wameikataa CCM na kuukataa uchaguzi wa marejeo Visiwani Zanzibar. Rejea: #Pemba wameikataa CCM,inatakaa uchaguzi wa marudio Zanzibar.Wapo walionielewa. Wapo walionipuuza. Wapo walioniponda bila ya kunipenda. Sasa mambo yanakuwa dhahiri.
Kadiri tarehe ya uchaguzi inavyokaribia,Zanzibar kunazidi kuchafuka. Nyumba na Ofisi zachomwa. Wananchi wanashambuliwa na kushambuliana. Hali tete. Ingawa viongozi wanadai na kuahidi kuwa hali ni shwari,tunashuhudia kinyume chake. Panazidi kuchafuka.
Natoa wito uchaguzi wa marejeo uhairishwe hadi hali ya amani Zanzibar itengemae. Hatuna haraka kama Taifa. Muda ni huu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Mh. Jecha, moja ya vigezo vya kufuta uchaguzi wa tarehe 25/10/2015 ni wajumbe kutofahamiana kiasi cha kurushiana ngumi na wananchama wa CCM kufanyiwa fujo huko Pemba.
Kwa sasa hivi hali ya Zanzibar hasa Pemba ni tete, ndiyo maana Polisi na majeshi yamerundikana huko. Nasikia na mabomu yanarushwa. Hii ni zaidi ya ngumi na kupelekea kuwa kigezo tosha cha kuahirisha uchaguzi kabla ya kuufuta tena. Mabomu na risasi vinamadhara makubwa kwa uchaguzi kuliko ngumi uliyopigwa na wajumbe wenzako kwenye tume unayoiongoza! Unadhani mugerushiana risasi ungekuwepo?
Ushauri wangu, Ili kuepusha kuufuta tena ni muda muafaka sasa ukaahirisha uchaguzi mpaka 2020. Sasa kama uchaguzi uliokuwa na askari kiduchu uliokuwa wa amani na utulivu uliuita wa machafuko vipi huu uliojaa sakari kiasi kwamba ratio ya askari kwa raia ni 1:1?
Kwakuwa ajenda ni CCM kutawala, njia rahisi nikuhairisha tu uchaguzi mpaka 2020 ili kunusuru raia wasiokuwa na hatia wala hawana mpango wowote wa kutembelea ikulu. Ilimradi uhakikishiwe ulinzi wa milele, au uhamie bara. Mambo ya katiba achana nayo, kama kuikanyaga iliisha kanyagwa vyakutosha. Acha wananchi waendelee na shughuli zao na majeshi yarudi yakaendelee na kazi nyingine.
Wale wateule wa Masheha na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waapishwe, tuanze ukurasa mpya.
Ila sasa Dr Sheni, hakikisha unaondoa wote waliokupotosha katika jambo hili na andaa mazingira ya CUF kutawala baada ya 2020.