Wito kwa Wizara ya maji

Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,359
697
Naomba kutoa wito wangu kwa wizara ya maji kwamba ni wakati sasa ifikirie kuchukua maji mto rufiji kwa ajiri ya wilaya za Ilala, Temeke, Mkuranga, Rufiji, Ikwiriri, na maeneo jirani. Nasema haya kwa sababu mto Ruvu umeelemewa na kina chake ni kidogo kwa hiyo unaweza hudumia wilaya za Kibaha, bagamoyo, Kinondoni, ubungo na maeneo jirani.

Kwa nini kama nchi tunang'ang'ania mto ruvu ili hali sehemu kubwa ya jiji la dsm ingehudumiwa na mto rufiji?? Prof. Mkumbo tafadhali anza na mawazo mapya........
 
Maji Dar Es Salaam Sio Tatizo.
Maji yanayopatikana Kutoka Ruvu toka juzijuzi walipofungua ule mtambo mwingine ni mengi kuliko yanayohitajika jijini.
Tatizo lililopo sasa ni Distribution ya maji kwenye nyumba za watu na sio Maji kufika DSM au kuisha RUVU.
 
Nimesema hayo kwa sababu mwaka jana Ruvu iliishiwa maji kwa sababu ya ukame ndo maana ni vizuri tufikirie vyanzo vipya vya kudumu!! kwanini Ruvu tuu?? Fikiria utoe maji ruvu yavuke jiji lote uyapeleke Mkuranga, hapo umefikiria au basi tu kwa sababu hakuna mawazo mapya??
 
Mawazo mazuri,
nilichokuwa naongezea ni kwamba shida ya maji DSM kwa sasa sio SOURCE ya maji bali ni DISTRIBUTION kwa watumiaji.
Hata kama wakienda Rufiji(Kama ni Feasible) au Ruvu hapohapo wakajenga water storage au Bwawa, bado Tatizo liko palepale. Mawazo mazuri mkuu ula tuangalie zaidi Tatizo lililopo tunalitatiaje zaidi...
 
Pamoja sana. Binafsi nakereka kuona nchi kama yetu yenye kila aina ya vyanzo vya maji eti wananchi tena ktk mji mashuhuri wa kibiashara wa nchi hawana maji.
 
Ni matarajio yangu kwamba Prof. Mkumbo amepata ujumbe huu.
 
Back
Top Bottom