Say no to actors
JF-Expert Member
- Aug 9, 2016
- 637
- 641
Ndugu wana jamvi kuna siku nilipost Uzi juu ya dhamira ya kuanzisha movement kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Kuna waliounga mkono na kusema ni jambo njema na kuna waliobeza na wengine kudiriki kusema katiba mpya siyo hitaji la watanzania.
Lakini mm nazidi kusisitiza kuwa mtu huwezi kujigamba kuwa unapigana vita dhidi ya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka wakati wewe mwenyewe uko chini ya mfumo unaopelekea hayo yawepo.
Tatizo la ufisadi Tanzania siyo mtu au aina ya uongozi bali ni mfumo uliowekwa na katiba mbovu iliyopo. Ubovu wa kwanza ni kibga ya kikatiba dhidi ya rais kutoshitakiwa. Na ukiona aina nyingi ya ufisadi uliokwishafanyika hapa nchini mhusika mkuu ni Rais.
Mahakama ya mafisadi itashindwa kufanya kazi kwa kuwa kila aina ya kesi kubwa itakayokuwa inapelekwa ktk mahakama hii mhusika mkuu na mshitakiwa namba moja atakuwa ni huyu aliye na kinga.
Na badala yake mahakama itakosa kesi ya kusikiliza na wakati tunajua tosha wahusika wa EPA,Richmond, Escrow, Dowans, samaki wa magufuri, nyumba za serikali, Buzwagi, ni gawa wahusika wapo na wengine ni viongozi mpaka leo na hawatoweza kujichukulia hatua.
Ili taifa letu liondokane na Rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka ni kuwa na katiba isiyoangalia maslahi ya chama, mtu yeyote au kiongozi bali tuwe na katiba itakayotanguliza mbele maslahi ya taifa na rasirimali zake. Pia kuwe na katiba itakayotupatia tume huru ya uchaguzi.
Tume huru ambayo kila mdau ataona ni huru kweli kweli. Na hivi vitu viwili haviwezi kuja kwa hisani ya mtu aliyeko kwenye mfumo juu dhaifu bali vitapatikana kwa vijana wote kujivua ukada na ushaabiki wa vyama na kuvaa koti la Tanzania mpya.
Movement siyo kosa kwamba utakamatwa na jeshi la polisi na kunyimwa dhamana movement ni haki yako na hasa pale malengo yake yanapoonekana kuwa chanya kwa ustawi wa taifa. Hatuundi movement ya kuiondoa serikali madarakani bali ni movement ya kuipata katiba makini kwa ustawi wa taifa pamoja na kupata tume huru ya uchaguzi.
By
Chogero Abdallah
From Arusha