makoye2009
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,638
- 1,218
Wana JF,
Kuna habari za kuaminika kutoka vyanzo vya ndani ya Bunge kwamba huyu Mama Tulia Ackson Naibu wa Spika anatafakari kujiuzulu mapema kabla ya kupigiwa kura na Bunge la JMT ya kutokuwa na imani naye.
Habari kutoka kwa watu walio karibu na mama asiye-TULIA zinanyetisha kwamba baada ya kutafakari na kupewa ushauri na watu wake wa karibu yuko kwenye hatua za kutangaza kujiuzulu. Hii ni kwasababu kitendo cha kutaka kupigiwa kura ya kumng'oa kutokana na Wabunge wote wa upinzani na wachache wa CCM kuona umuhimu wa kufanya hivo.
Mmoja wa washauri wake wa karibu amesema kuwa itakuwa ni aibu sana kwa Tulia Ackson kama ataondolewa kwenye Unaibu spika kwa kupigiwa kura na itakuwa ni historia na mara ya kwanza kutokea tangu Bunge la Tanganyika na baadaye Tanzania lianze. Uwezekano wa kupigiwa kura nyingi ya kutokuwa na imani naye unawezekana kuwepo kutokana na baadhi ya Wabunge wa CCM kuwa na manung'uniko ya chinichini kuwa huyu mama hatakiwa na aliingia Bungeni kwa kulazimisha kupitia uteuzi wa JPM huku akiwa hana sifa kabisa ya kuwa Mbunge, N/spika au Spika kwa vile hana historia wala hajawahi kuwa mwana chama wa CCM wala Mkuu wa Wilaya au Mkoa na hivo kuonekana kupwaya na kuyumba sana anapokuwa kwenye kiti.
Tangu mama huyu aanze kuongoza Bunge hili wakati Spika Ndugai hayupo kumekuwa kukitokea vurugu na kutoeleawana ndani ya Bunge kati yake na Wapinzani na huku akionyesha chuki za waziwazi kanisa kuwa hawataki Wapinzani kitu ambacho si sahihi kwenye taratibu za Mabunge yenye sera za vyama vingi.
Kuna matukio ambayo hata Wabunge wenzake wa CCM wameona hayawafurahishi kama vile kujichukulia maamuzi peke yake bila ushauri wa Spika na Bunge lote kwa ujumla. Wabunge wa CCM wanasema kitendo cha Tulia Ackson kuchukua fedha ya Bunge kiasi cha 6 Bilioni na kuzirudisha Hazina kupitia kwa JPM kimewakera Wabunge wengi wa CCM akiwemo Spika Job Ndungai mwenyewe na kuapa kumng'oa haja-TULIA. Kitendo hicho kimewasababishia Wabunge wengi matatizo kukosa au kutopata posho zao kwa wakati kwasababu ya unafiki, ukimbelembele wa kujikomba kwa Raisi JPM.
Hivo wame apa kwamba kama hatajiuzulu kuepuka aibu ya kung'olewa kwa nguvu basi wataungana na wenzao wa UKAWA kumshikisha adabu bi Tulia.