Wito kwa RC Dar: Tuondolee Ujambazi DSM

Donyongijape

JF-Expert Member
May 28, 2010
1,497
812
RC Makonda,

Ningependa utambue pamoja na kwamba Raisi ameteua Majenerali kwenda mipakani kwa concern ya usalama, ujambazi unaofanyika huko, haufikii unaofanyika Dar hata Kidogo. Hasara ya Ujambazi huu ni mkubwa sana kwa Amani na Uchumi wa Wana DSM, na Wageni wake.

DSM imejaa ujambazi wa bodaboda, uvamizi wa maduka ya wajasiliamali especially Kata Ya Goba, Madale, Chnika, Mbagala etc, Uvamizi wa Nyumba za Watu Binafsi maeneo mbali mbali, Vibaka Wadogo wadogo, Panya Road, na Uvamizi wa Mabenki.

Naamini hii kwa ujumla wake, inarudisha nyuna maendeleo ya Wana Dar es lama wengi.

Nakuomba, hili Liwe kipaumbele chako, Onyesha ubunifu na Ukakamavu, waprove wrong kuwa Mwenyekiti wa Usalama ni Lazima awe Mwanajeshi.

Ondoa Ujambazi Dar, Okoa Maisha ya Wana Dar es salam, rudisha Amani Dar, Rejesha usalama Dar. Usalama wa Dar upo Mikononi mwako kama Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama.

Wana JF mnaoishi Dsm. TUSHIRIKIANE KUFIKISHA UJUMBE HUU.

UPDATE: 17/03/2015
Makonda ametangaza siku 90 za wenye silaha kusalimisha. Hii ni hatua nzuri ya kuanzia. Ongeza speed baba, tunahitaji DAR Salama kabisa.
 
RC Makonda,

Ningependa utambue pamoja na kwamba Raisi ameteua Majenerali kwenda mipakani kwa concern ya usalama, UJAMBAZI unaofanyika huko, haufikii unaofanyika DAR hata Kidogo. Hasara ya Ujambazi huu ni mkubwa sana kwa Amani na Uchumi wa Wana DSM, na Wageni wake.

DSM imejaa ujambazi wa bodaboda, uvamizi wa maduka ya wajasiliamali especially Kata Ya GOBA, MADALE, CHANIKA, MBAGALA etc, Uvamizi wa Nyumba za Watu Binafsi maeneo mbali mbali, Vibaka Wadogo wadogo, Panya Road, na Uvamizi wa Mabenki.

Naamini hii kwa ujumla wake, inarudisha nyuna maendeleo ya Wana Daresalama wengi.

Nakuomba, hili LIWE kipaumbele Chako, Onyesha ubunifu na Ukakamavu, waprove wrong kuwa Mwenyekiti wa Usalama ni Lazima awe Mwanajeshi.

Ondoa Ujambazi Dar, Okoa Maisha ya Wanadaresalama, Rudisha Amani Dar, Rejesha Usalama Dar. Usalama wa DAR upo mikononi mwako kama Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama.

Wana JF mnaoishi DSM. TUSHIRIKIANE KUFIKISHA UJUNBE HUU.
Umesema kweli,

Dar ina changamoto nyingi ukiondoa huo ujambazi wa wazi
bado kuna ujambazi uliojificha nyuma ya mgongo wa sheria
kama vile ule wa UDA kuhodhi route ya kwenda ferry/kigamboni soko la samaki na kituo cha kupandia pantoni.

Zamani mtu ulikuwa unalipa 500.00 yako toka Tabata hadi ferry,siku hizi
ni lazima wala siyo utashi kushuka mnazi mmoja na kuamua ama upande UDA au utembee kwa mguu hadi ferry.

je huu sio ujambazi? Nini maana ya ushindani wa kibiashara?
kwanini UDA asitengeneze mazingira mazuri ya abiria kuyapenda magari yake
badala yake anatengenezewa mazingira ya watu kulazimika kulipa nauli mara mbili

Ili wafike waendako.
Naomba na hili Makonda uliongeze ili kukomesha ujambazi uliohararishwa na mamlaka husika.
 
Ni pendekezo zuri kwa mkuu wa mkoa, ila tatizo la ujambazi Dar ni ngumu kumalizwa na RC hata awe mpya. Atakachoweza ni kupambana siku 2 tatu za mwanzo ili aonekane kwenye kamera, lakini baada ya hapo itakuwa business as usual. Katika mlundikano mkubwa wa watu kwa kiwango hicho tena zaidi ya nusu wana kazi zisizo rasmi ni rahisi sana wahalifu kujichanganya hapo na kufanya mambo yao.

Anachoweza kufanya tena hili sio yeye tu kwani ni tatizo la kitaifa ni serekali yetu kuwekeza nguvu kubwa kwenye kilimo kwani ndio ajira nyingi zilipo.

Huko kukiboreshwa wangalau 1/3 ya watu wa Dar watarudi vijijini
kujishughulisha na kilimo, na hali hii itapunguza vijana wasio na kazi rasmi hapo jijini. Kinyume na hapo ataishia kujitahidi siku za mwanzo lakini baada ya muda mfupi atachoka.
 
Kwa nimuonavyo akili yake yote iko kwenye namna atakavyopata Uwaziri baada ya kunyanyasa wapinzani.Priority yake ni kuhakikisha wapinzani wanakiona cha moto
 
Kwanza kabisa nakupongeza kwa kuteuliwa , wewe kama kijana unatakiwa kuondoa ombaomba wa barabarani na hata wa kwenye mabaa yaani wakongo na wamanyema waliochoka kimziki ifika hatua bendi za kikongo zipewe mwaka kama hazina pissue marudi kwao sio kujazana kwenye mabaa kusifia majambaz na matapeli
 
Kwa nimuonavyo akili yake yote iko kwenye namna atakavyopata Uwaziri baada ya kunyanyasa wapinzani.Priority yake ni kuhakikisha wapinzani wanakiona cha moto
Wapinzani nao ni watu au??? Huwa sioni kabisa umuhimu wao....si ushaambiwa wao wakienda mjengoni wanagongeana glass.....na kukenuliana meno.
 
Ameanza vizuri kwa kutoa onyo hili la siku 90

Lakini alitakiwa kuwaambia kwa wale ambao hawajarenew leseni zao wafanye hivyo kabla ya Siku tisini.

Kama siku moja kabla haja sema nimesharenew leseni yangu kwa nini nirudi tena polisi.

Polisi wana list ya hao wenye leseni. Tusipende kama mabogi mabovu kuna Teknolojia za kisasa ambao dakika tu polisi anaweza kujua ni wangapi wamesharenew wanagapi bado na lini wanatakiwa kurenew.

Maana kila mtu Ana siku tofauti ya kupata leseni hiyo
 
Hivi huyo Makonda wenyu alipitia angalau mafunzo ya UKAKAMAVU au MIZUKA inatoka juu inawapanda na walio chini siku hizi.

Ikumbukwe MAJAMBAZI siyo vibaka wa karakoo au mateja wa kwa manyanya.
 
Back
Top Bottom