Alexism
JF-Expert Member
- Aug 14, 2011
- 3,423
- 2,046
Bila shaka hakuna Mtanzania ambaye anaupenda ufisadi maana ni janga kubwa kwa Taifa letu.CHADEMA ikiongozwa na Dr.Slaa walifanyakazi kutuonyesha kwa vitendo kuupinga ufisadi kwa kuwataja washiriki wakubwa wa ufisadi ili ni mmoja tu ambae alikubari kutubu na kuachana na chama cha mapinduzi kwakua inasemekana kua ndio chanzo na shule ya ufisadi.Sasa kama kweli CCM inauvua au kuuchukia na kupinga ufisadi basi ni wakati muafaka wa kuwafukuza na kuwanyanganya kadi wote waliotajwa pale Mwembe Yanga tukianza na J.Kikwete,B.Mkapa,N.Mkono,A.Chenge,R.Aziz,N.Karamagi etc
CCM mkifanya hivyo basi mtakua mmetudhirishia kua mnaupinga kwa nguvu ufisadi na mtaaminiwa sana lakini bila kufanya hivyo basi nadiriki kusema kua CCM na ufisadi ni Doto na Kulwa.
CCM mkifanya hivyo basi mtakua mmetudhirishia kua mnaupinga kwa nguvu ufisadi na mtaaminiwa sana lakini bila kufanya hivyo basi nadiriki kusema kua CCM na ufisadi ni Doto na Kulwa.