Wito - CCM ijitathimini mara moja

MNYOO JOGOO

Senior Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
195
Reaction score
94
Tukiwa tumeshuhudia kumalizika kwa chaguzi za udiwani katika mikoa mbalimbali nadhani sasa ni wakati wa chama tawala kukaa na kutafakari wapi imekosea na wapi ijirekebishe ili dhahama hizi zisitokee siku zijazo. Mhimu iangalie kama mapokezi ya vijana wanaojiita wapambanaji waliohama kutoka chadema na kujiunga CCM kwa publicity kubwa na hamasa huku mwenyekiti akijivunia vijana hawa kwa furaha kuliko hata mapokezi mfalme mswati alipokuja kufungua maonyesho ya 77 KAMA kweli jukumu walilopewa wamelitimiza kadri ya matarajio ya muongozo wa chama.

Sitaki nizungumzie jinsi vijana wazuri- CCM walivyopokwa majukumu na kukabidhiwa mtoto wa kambo, huku tukitarajia kuvushwa katika dhoruba kubwa hili la kisiasa ambalo upinzani hususani chadema wameonekana kujidhatiti. Umoja wa vijana walibaki wakisoma magaziti ya uhuru wakati mwingine wakisali mioyoni mwao kuombea mambo yaende ndivyo sivyo ilimradi nyoyo zao zisuuzike kwani walijihisi kutengwa kwani majukumu ambayo walidhani ni haki yao kuyafanya sasa yalifanywa na wa watoto wa kambo.

Rafiki yangu aliniuliza hawa ni kina nani hata wapewe kipaumbele namna hii? Nikamuambia muulize mwenyekiti!

Makosa haya yasijirudia katika chaguzi zijazo - kwani kuwa na mtaji wa vijana ambao badala ya kuuzasera nzuri ya chama wanakuwa na mashambulizi personal kwa mpinzani as if bado wanamapenzi na chama icho ila ndoto zao zilikatishwa tu.
 
Tumejifunza madharaya usaliti,hao waliowekwa mstali wa mbele katika mapambano ya CCM kule Arusha ni wale waliofukuzwa CHADEMA Mbeya kwa usaliti. Ukisajiliwa kwa mkopo siku timu uliyosajiliwa kwa mkopo ikicheza na timu yako ukaanza kufingisha magoli ni kwamba unajiharibia zaidi maana hata timu yako itadhani kuna siku utafanya hivyo hivyo kwao;

Ndio maana CHADEMA haihitaji wanaohamia toka CCM, CCM cha kujifunza ni wasaliti siyo mtaji, kwani Tambwe Hiza aliwafikisha wapi?Mwigulu aache strategy zake mbovu za kutembeza wahanga, hizo ni cheap politics
 
Ni kweli, CCM ijitathmini, iachane na siasa za maji taka na badala yake wafanye siasa za kisomi.. Tunahitaji CCM kama chama cha kisiasa na siyo kama genge la mauaji kama kinavyojidhihirisha sasa...

Mungu Ibariki Tanzania.
 
wataachaje siasa uchwara wakati hawana sera
 
wataachaje siasa uchwara wakati hawana sera

Trust me, watu wenye akili timamu na wanaoitakia mema CCM wapo...
Kuna washamba wachache ambao wamekihodhi Chama na wenye akili wamepuuzwa....
Siasa za ushindani ndicho kitu ningependa kuona kinatokea hapa Tanzania, bila kuumizana wala kutukanana...
 
Very True
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…