Windows phone vs android niende wapi?

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Posts
32,062
Reaction score
43,487
Ni kawaida sasa hivi kwenye redio kusikia matangazo ya lumia, samsung galaxies zinazidi kushika kasi, techno wanakomba soko la Tanzania na huawei nyingi za tigo zinazidi kusambaa. yote haya yanaweza kukuchanganya na kufanya usifanye uamuzi sahihi wakati wa kuchagua simu. hebu tuangalie windows phone ni nini na android ni nini na baadae utajua ufanyeje kuchagua simu sahihi.

Windows phone 8
Hii ni operating system iliyotengenezwa na microsoft inatumika kwenye simu za nokia, htc, samsung na huawei mpaka sasa. imekuja kumreplace windows phone 7 ambayo haikupokelewa vizuri na wateja. tofauti na android windows phone inatumia tiles badala ya icon design yake hii imeipa umaarufu sana.


Android
Hii ni operating system iliyotengenezwa na google na inatumika na watengeneza simu zaidi ya 80 wachache wao ni samsung, htc, huawei, tecno, sony, lg na asus. Hii inatumia icon tofauti na windows phone. pia ina homescreen ambayo unaweza kueka app zako unazozipenda.

Je ukitaka kununua simu ya windows phone uangalie nini?

Its about people vs apps
Kitu kimoja kizuri kuhusu windows phone ni uwezo wake wa kukusanya watu wote unaowajua na kuwaweka pamoja na kukupa habari zao zote. kuna peoples hub ambayo inakua na list ya marafiki zako na kama wana acount za facebook, twitter, unaona habari zote kwenye contact bila hata kufungua app ya twitter au facebook.

Ukitoa peoples hub kuna feature kama kids corner ambayo ni simu ya mtoto ndani ya simu yako, hapa unachagua application, video, miziki ambayo unataka mtoto wako aone akishika simu ili kumzua asifanye vitu vibaya. pia kuna rooms ambayo inakua ni private area kati yako na watu unaowapenda kama mke wako na wakwe zako eneo ambalo mtashare location na kila kitu. haya na mambo mengi yanaifanya windows phone kua very strong kwenye upande wa watu.

One thing cool about android ni ina application nyingi sana. so far kuna application zaidi ya 700,000 wakati windows phone ina application 150,000 tu. hili linafanya vichwa vikubwa kama instagram kupatikana android na kukosekana kwenye windows phone.


So wakati unachagua simu uangalie mahitaji yako kati ya hivyo vitu viwili hapo juu.

Its about microsoft vs google
Kuna msemo siku hizi kuwa hununui simu bali unanunua ecosystem. huu msemo ni sahihi kabisa kwani kila platform siku hizi ina apps zake ambazo ni exclusive kwao tu, hapa nitaelezea ecosystem inayopatikana kwenye android na windows phone. kupunguza ukubwa wa thread nitazimention tu kama utataka maelezo zaidi utacoment

  • microsoft office(wp) vs quickoffice(android)
  • search (bing search) vs search (google search)
  • map (nokia,bing map) vs map (google map)
  • video (hakuna) vs video (youtube)
  • mail (outlook,hotmail) vs mail(gmail)
  • cloud(skydrive) vs cloud (google drive)
  • video chat(skype) vs video chat (hangout)
  • gaming (xbox) vs gaming (hakuna)
Hizi ni chache za muhimu so utaangalia ecosystem ipi unaipenda hapa nimeexclude apps za nokia maana ni special case.

Its about design vs customization
Kama nilivoelezea hapo juu windows phone imekuja na design mpya kabisa ya tiles ambazo ni live zinakupa information papo kwa hapo hizi tiles huwezi kuzichange na kuweka customization kama android lakini unaweza eka design unayotaka. unaweza resize tiles zikawa kubwa, za kati au ndogo na pia unaweza ukachange skin.


Andoid yenyewe ipo vizuri kwenye customization kuliko windows phone unaweza ukaieka home screen yako the way unavyopenda wewe. zipo launcher mbali mbali zenye themes tofauti tofauti kwa kazi hii. kwenye android pia kuna launcher ambazo zinakuwezesha kuweka themes za 3d ili kuwezesha wewe kufeel tofauti ukitumia simu


Its about security vs freedom
Kwenye windows phone mpaka sasa huwezi kuroot simu wala kufanya hacking ya aina yoyote simu imefungwa kila kona hili linaongeza ulinzi kwenye simu yako hutaathiriwa na virusi wala malware wa aina yoyote device itakua salama lakini tatizo linakuja unakosa uhuru hutaweza kufanya vitu unavyotaka wewe.

Kwenye android unakua huru unaroot simu unaeka custom firmware unafanya vitu unavyotaka wewe lakini tatizo linakuja kwenye security android kuna malwares wengi wanaweza wasiwe virusi lakini vitu kama spyware na adware ni vigumu kuviepuka kwenye android.


its about productivity vs playing
nafkiri hapa ndo pa muhimu zaidi panapozitenganisha hizi simu. kuwepo kwa microsoft office, skydrive, photobeamer, security kubwa, offline navigation na simu kuwa fasta kunaifanya windows phone kuwa nzuri kwa wafanya biashara kuliko android.
kuwepo kwa HD games, na application mbali mbali kunaifanya android iwe simu nzuri ya kuchezea so hapa unatakiwa uangalie unahitaji nini je wewe unapenda kuchezea simu au unataka simu yako iwe productive? maana unaweza ukaenda windows phone then ukakuta games chache ukaanza kulalamika. na unaweza kuwa mfanya biashara ukaenda android ukaanza kulalamika betry na simu kuwa slow.

Hayo ndio mawazo yangu kuhusu windows phone na android nikiwa kama mtumiaji ambaye nishatumia platform zote. pia kuhusu windows phone nimeongelea windows phone 8 na sio 7 better unaponunua simu ya windows phone ununue 8, kama huna uhakika ni vizuri uulize.
 
daaah very nice bro, thanks kwa kutupa maujuzi....ila hapo ungeongeza na kakipengele ka kuiongelea iOS ungekuwa umemaliza kazi kabisa
 
daaah very nice bro, thanks kwa kutupa maujuzi....ila hapo ungeongeza na kakipengele ka kuiongelea iOS ungekuwa umemaliza kazi kabisa

tatizo ios ni bei mkuu wachache humu wanaoweza kuzimudu then pia mimi ios nimetumia simu za watu tu sijamiliki mwenyewe sipo familiar sana na hii os
 
hapo kwenye video chat skype pia unaweza kuidownload katika android na ikafanya kazii vizuri tu,by the way big up kwa analysisi yako imetulia mno,as far as i know window 8 inapata update hune 26th inaenda kuwa 8.1 na kuna tetesi kwamba start button itarudishwa vipi kuhusu kwenye simu upadte hiyo itapatikana pia???
 

mkuu hata youtube ipo kwenye wp hapa naelezea ecosystem skype kwenye wp inakua integrated kabisa wakati kwenye android hadi udownload app. kwenye youtube nako wp hamna official app ya youtube itabidi uhangaike na 3rd party app kama metro tube so vitu kama hivi vinaharibu ecosystem ndo mana sijaeka.

kuhusu blue update(8.1) kwenye windows phone tetesi vitaongezeka hivi
1. fm radio
2. double tap to awake
3. tiles nyingi zaidi (zaidi ya 3 kwa upana)
4. kusuport google sync
5. data sense kusuport more carier
 
Mkuu
heshima yako napata ujuzi zaidi toka kwako
viva Chief Mkwawa
 
mkuu unataka kuniambia kwenye hiki ki xperia changu naweza kudownload skype ikafanya kazi kama kawa!!!

yah mkuu unaweza android haina limitation ya apps as long as una os inayokubalika. japo perfomance inaweza kuwa sio nzuri. ni xperia ngap ngap?
 

The world of apps available in Android's Google Play is too big to miss.....I am Droid fun...
 
...

kuhusu blue update(8.1) kwenye windows phone tetesi vitaongezeka hivi
1. fm radio
2. double tap to awake
3. tiles nyingi zaidi (zaidi ya 3 kwa upana)
4. kusuport google sync
5. data sense kusuport more carier
mkuu nikichukua Lumia nitapata skype tayari ikiwa ni sehemu ya simu?
 
mkuu nikichukua Lumia nitapata skype tayari ikiwa ni sehemu ya simu?

mkuu whether inakuja na simu au utaidownload vyote inawezekana lakini cha muhimu hapa ni integration mfano ukiwa katika peoples hub unapiga simu kwa skype bila kuopen app ya skype
 
halaf nasikia tecno n3 znakuja na skype is real?

mkuu skype wana version ya android inamaana simu yoyote inayotumia android inauwezo kurun skype (sjajua kuhusu version za android za zamani)

so mkuu itarun as long as ni android sema ustegemee quality ya video na picha iwe kama ya galaxy s4 na htc one
 
ahsante mkuu kwa mwongozo huu mzuri. kama utaweza ningeomba ututajie na makadirio ya bei za simu zake hasa kwa makadirio ya chini yaani ya bei nafuu.
 
ahsante mkuu kwa mwongozo huu mzuri. kama utaweza ningeomba ututajie na makadirio ya bei za simu zake hasa kwa makadirio ya chini yaani ya bei nafuu.

lumia 520 ndo cheapest kwa windows phone 8 around 260,000 hadi 350,000 wakati kwa android zipo nyingi nyingi tu around 150,000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ