windows 7 all editions

windows 7 all editions

Mc Donald

Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
21
Reaction score
3
hivi kuna tofauti yoyote kati ya windows 7 starter, home, proffesional na ultimate?
nn tofaut yake, na ipi nzuri zaidi?
 
hivi kuna tofauti yoyote kati ya windows 7 starter, home, proffesional na ultimate?
nn tofaut yake, na ipi nzuri zaidi?

Tofauti ni kubwa sana ndugu, hizo editions zote zimetengenezwa kwa ajili ya watumiaji tofautitofauti. Kwa hiyo ni hiyari yako kuchagua Windows itakayoendana na mahitaji yako.

1. Windows 7 Starter
Hii ni edition ya Windows ambayo ina features chache zaidi, na ipo kwa 32 bit version pekee. Imekosa vitu kama ile Aero Transparency, visual styles pamoja na kubadili Desktop wallpaper. Mara nyingi utaikuta hii edition kwenye Netbooks ambazo zipo kwenye masoko ya pc's.

2. Windows 7 Home Basic
Hii ni version ya Windows ambayo pia imekosa baadhi ya features, pia hii inashindikana kufanya activation kwa baadhi ya nchi. Hivyo imepewa kiwango maalum.

3. Windows 7 Home Premium
Hii ni edition ambayo imelengwa hasa kwa matumizi ya nyumbani, ikaja na features kama Windows Aero Transparency pamoja na Windows Media Center.

4. Windows 7 Professional
Hii ni Windows kwa ajili ya Watu wenye biashara ndogo, watu wenye matumizi ya kiofisi pamoja na wale wenye shauku na hamu ya kuitumia hii editions kutokana na kutoridhika na Edition za nyuma. Hii Windows ilikuja na feature ya ku-support mpaka 192 GB ya RAM. Features nyingi e ni kama kubackup network location pamoja na file system encrypting.

5. Windows 7 Ultimate
Hii ndiyo edition ya Windows inayobeba features zote za edition za nyuma za Windows 7. Feature nyingine ni kwamba pia hii inapatikana kwa watumiaji wa nyumbani kwa single license.
 
DddfOK
hivi kuna tofauti yoyote kati ya windows 7 starter, home, proffesional na ultimate?
nn tofaut yake, na ipi nzuri zaidi?
  • Ultimate ni nzuli.
  • Kwa mtumiaji wa kawaida ukiondoa STARTER, hutoweza ona tofauti baina ya hizi windows
Zaidi | Windows 7 editions
 
  • @dreamchaser naona hapa tumetofautiana katika kubofya SUBMIT REPLY @07:24am
 
asante, nilikuwa natumia starter, nikataka ku upgrade mtu mmoja akaniambia hakuna tofaut yoyote, ss naweza ona kuna utofauti.. nita upgrade to ultmt!
 
Back
Top Bottom