Wimbo wa Taifa: Kwanini tubarikiwe?

Wimbo wa Taifa: Kwanini tubarikiwe?

MADINI CHUMA

Member
Joined
Dec 25, 2013
Posts
29
Reaction score
9
Ndugu wanaJF, mara nyingi huwa nafikiria waliotunga wimbo wa taifa walimaanisha haya tunayoyaona au mengine yasiyotendeka? Tanzania inaviongozi ambao wako tayari kushuhudia wananchi wao wanakufa kwa kukosa madawa wakati wao wanawaibia mabilioni ya hela halafu tunaimba Mungu ibariki, Viongozi wanawambia wananchi wao ni bora wale nyasi wao wapate kusafiri kwa ndege, Viongozi wanawaambia wananchi wao wapige mbizi kama hawawezi kulipa nauli kizukoni, Viongozi wanasema mikataba ya madini itabaki kuwa siri utadhani hii nchi ni mali yao, Viongozi wanaiba mabilioni ya pesa wanasema ni vijisenti wakati kuna wamama wengi wajane wanashindwa kuwapeleka watoto wao shule kwa kukosa ada na michango mingine, Viongozi wanawalazimisha wananchi wachangie ujenzi wa maabara wakati wao wanaiba mabilioni ya hela na hawakotayari kuwasaidia, Ndugu zangu, kwanini Mungu atubariki wakati hatutaki kufuata aliyotuagiza? MUNGU WASHUSHIE LAANA WOTE WANAOWAIBIA MASKINI MALI ZAO NA KUNENEPESHA MATUMBO YAO.
 
Hakika na kweli Mungu akitaka kutubariki akaangalia Tanzania akakuta mafisadi ndo wameshikilia uchumi wetu anaweza kughaili.EEEEEEE Mungu tusaidia.
 
Kuna mkazi mmoja nadhani yupo Kisarawe alitoa maoni yake kwenye tume ya Warioba kuwa wimbo huo ufutwe kwakuwa unasema "Mungu ibariki ......., wabariki viongozi wake....., kwanini Mungu awabariki wezi???
 
Back
Top Bottom