Wimbo Wa "Mfalme" wa Belle9

mpuyango

Member
Aug 17, 2016
60
68
Msanii anayeiwakilisha vyema mji kasoro bahari Morogoro Belle9 ameachia ngoma yake mpya inaitwa "Mfalme", kwa upande wangu ni ngoma kali japo ngoma imeachiwa tu mitandaoni hope ikiachiwa redioni pia itapata rotation ya kutosha. Lakini bana asubuhi nilikuwa nasikiliza huu wimbo nikakumbuka Miaka mitatu nyuma MwanaFA alishawai kuachia ngoma yake yenye tittle kama ya belle9 "Mfalme" ambapo alimshirikisha G.nako ilikuwa ngoma kubwa na ile corus ya G.nako ni moja kati ya corus kali kuwai kutokea kwenye mziki wa bongoflava. Lakini uzuri ni kwamba hatujamsikia mwanaFa wala mashabiki wake wakicomplain kuhusu hicho kitu kwa sababu kwenye mziki tittle ya ngoma kufanana ni jambo la kawaida mno. Sasa nilikuwa nimekaa nikafikiria kwa akili yangu ndogo nikajiuliza hivi ikitokea Siku Diamond Platnumz ametoa wimbo unaoitwa labda "Mwana" au "chekecha cheketua" au itokee Alikiba atoe wimbo unaitwa "Nitampata Wapi" au "Eneka" Itakuwaje?

Nawasilisha!

Sent from my GT-S7580 using JamiiForums mobile app
 
Baadhi ya mifano yako imenifurahisha japo sina mpango na hayo mambo ya Team Kiba, Team Diamond ila siku Diamond akitoa wimbo unaitwa Chekecha Cheketua mimi nitashtuka sana au Kiba atoe wimbo unaitwa Eneka, itashtusha.
kwanini hujashtuka kwa belle9 mkuu

Sent from my GT-S7580 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom