Wimbo wa Amani- Ulioimbwa jana

Wimbo wa Amani- Ulioimbwa jana

Akili Unazo!

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2009
Posts
3,930
Reaction score
4,934
wadau ,

Nawasilimu.
Naomba mwenye nakala ya wimbo ulioimbwa na kwaya moja jana juu ya Amani ambayo umepelekea Rais wetu kufanya maamuzi magumu ndani ya wiki hii.

Nawasilisha
 
Amani ni kauli mbiu ya watawala kutimiza matakwa yao ovu, watu wakigadhibika wanakimbilia neno amani amani. By the way, Jana ilidhihirika kabisa inchi Hii ni ya mfumo kristo.
 
wimbo wa kwaya AICT kutoka mwanza ".chezea pengine" ulivuta hisia za wengi , kikwete alivutika nao, aliupigia makofi , lowassa alijirusha ufahamu
 
Sema waimbaji sauti zao zilikuwa hazitoki. Sana sana nilikuwa nasikia sauti ya kwenye cd tu!!
 
Maudhui ya wimbo uitwao ‘Chezea
Pengine’ yanayokosoa
viongozi wasiojali wananchi
yaliamsha shangwe kutoka
kwa wananchi waliohudhuria
sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanganyika katika Uwanja
wa Uhuru, Dar es Salaam jana. Wimbo huo wa Kwaya ya AICT
Makongoro kutoka Mwanza
ulionekana kuwaingia wengi
ambao walitingisha vichwa
vyao na wengine kupiga
makofi kuashiria kukubaliana na maudhui yake. “Cheo ni dhamana, hakuna
aliyezaliwa nacho uliye
madarakani yapasa kusimama
kwenye haki wala
usijidanganye walio chini
hawajui kitu, haki ya mnyonge haipotei, bali
inacheleweshwa. “Keki inapokatwa kila mtu
aipate, hivyo inapogawiwa ni
vyema kila mtu aipate lakini
ikiishia juujuu elewa kwamba
chini manung’uniko yataanza,
mwisho wake ni vurugu, chezea pengine usichezee
amani,” ni miongoni mwa
maneno yaliyopo kwenye
wimbo huo. Waimbaji hao waliwataka
wanasiasa na waandishi wa
habari kutokubali kununuliwa
na kuwa chanzo cha kupotea
amani.
"Chanzo gazeti la mwananchi"
 
wimbo huu ulinigusa na kuniponyaaa,, kweli cheo sikuzaliwa nacho
 
Kwamba wimbo huo umemfanya Mheshimiwa afanye maamuzi mazito....mhhhh:confused2:
 
Mheshimiwa alikuwa anaimba huku akiona aibu aibu, kwa sababu alikuwa anautumia kama vitisho kwa watanzania ili wasihoji wizi wao walioufanya.
 
mie pia nataka kujua ntapata wapi wimbo huo.Kuna album ninunue au.
 
TBC I huwa wanaucheza sana kwenye TV. Video yake imechanganywa na ile waliyoshoot studio za TBC na ile ya Siku Kuu ya Uhuru.
 
Back
Top Bottom