Clouds siku hizi hawapati matangazo kama zamani.. mapato yakipungua maana yake posho za staff zinapungua pia... wafanyakaz wanaona wananyonywa...
Balaa lote hili limeletwa na mtoto wa tandale na wimbo wake wa mbagala uliomfanya tanzania tumjue na tumpokee..
Acha Uongo.
Sasa kama Clouds mapato yamepungua, Radio nyingine si ndio zinakufa kabisa.
Ukweli ni kwamba, watangazaji wengi pale Clouds hawana mikataba. Walichokuwa wanakifanya ni kutoa platform kwa mtu yeyote mwenye uwezo kuonesha uwezo wake kwa maana ya kutangaza bure, halafu utaambulia posho kulingana na wenyewe watakavyoona.
Vile vile, walitoa nafasi ya mfanyakazi yeyote pale kujiongeza na ikitokea ana kimradi cha pembeni then anaweza kutumia Radio kujitangaza bure.
Sasa inavyoonekana Kusaga na bahili hatoi hata posho wala hayuko karibu na wafanyakazi kama alivyokuwa Ruge. Fiesta yenyewe tangu Corona iingie haijafanyika.
Sasa mtu hawezi kukaa tu pale malipo yoyote. Pia kuhama au kuacha kazi ni kawaida, hakuna radio ambayo watu hawahami wala kuacha kazi. Hivi karibuni tu Jonijoo kahama Wasafi, Sam misago kaacha kazi EATV, Mpoki kaacha kazi Efm.
Vipi na huko mapato yakoje?
Huu mfumo wa kutumia watu bila malipo radio nhjngi zinautumia, ilamradi unapenda kuuza sura au kusikika radioni na unaweza weza unacjukuliwa. Sasa hivi EFM comedians kibao wamejaa pale hadi Kingwendu, sasa usidhani wameajiriwa kama watangazaji wanalipwa.
Pia kwa watangazaji wakubwa, nadhani wanatafuta namna ya kukua na maslahi kutokana na ukweli kwamba monopoly ya Clouds imepungua ( hata kama ni kidogo ) kutokana ujio wa Wasafi na Efm sokoni.
Na hii ndio maana wasanii na watangazaji wamepata aktenatives.