Wilbroad Slaa: Hakuna wa kumzuia Dk. John Pombe Magufuli mwaka 2020. Wapinzani wanaponzwa na kurukia kauli za viongozi badala ya ajenda

Daimler

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
556
973
IMG_8553.JPG


Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Wilbroad Slaa, amesema kuwa Vyama vya Upinzani nchini vinaweza kufutika katika ulimwengu wa siasa kwa kuwa, havina ajenda rasmi zaidi ya kurukia Kauli za Rais Magufuli.
Slaa aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, alisema kuwa, hakuna Chama kinachoweza kwenda Ikulu kwa kukosoa usahihi wa lugha wa lugha inayotumiwa have Viongozi walio madarakani kwa kuwa kauli ya mtu si ajenda inayoweza kuwashawishi watu."

IMG_8554.JPG
 
Huu ni ukweli mchungu..Me naamini katika Watanzania waliopo sasa Mwenye UWEZO wa kumtetemesha MAGUFULI 2020 ni Dr SLAA TU kama ikatokea AKAWA MGOMBEA 2020 na akaunda chama chake atapata WABUNGE WENGI MNO....huyu mzee still bado yupo kwenye MIOYO YA WAPINZANI WA KWELI
 
Huu ni ukweli mchungu..Me naamini katika Watanzania waliopo sasa Mwenye UWEZO wa kumtetemesha MAGUFULI 2020 ni Dr SLAA TU kama ikatokea AKAWA MGOMBEA 2020 na akaunda chama chake atapata WABUNGE WENGI MNO
Arudi basiii mm nimemisi siasa zake. Ijapo naaamin bado ile kadi ya kijani anayo.
 
Yeye kaona kauli tu ndio zinazokosolewa.Yeye amewahi kumkosoa kwa lipi?

Huko Ulaya na Marekani watu wanaandamaba kupinga matamshi au kauli tu zisizofaa za viongozi alafu yeye anataka kuona kauli za viongozi ni jambo dogo wakati wamebeba dhama kubwa!

Baaada ya kutoka CHADEMA alidhani chama kingekufa ila sasa anaona hali ni tofauti hivyo roho inamuuma.

Shariti mojawapo lisilotamkwa rasimi hadharani la wateule wa safari hii kupanda vyeo,kulinda vyeo na hata kupata uteuzi, ni kushambulia upinzani, kuhujumu upinzani na kujipendekeza kwa kuimba mapambio na kusifu na wala sio utendaji mzuri wa kazi.
 
Huu ni ukweli mchungu..Me naamini katika Watanzania waliopo sasa Mwenye UWEZO wa kumtetemesha MAGUFULI 2020 ni Dr SLAA TU kama ikatokea AKAWA MGOMBEA 2020 na akaunda chama chake atapata WABUNGE WENGI MNO....huyu mzee still bado yupo kwenye MIOYO YA WAPINZANI WA KWELI

Ukiwa vitani kamanda au mkuu wa kikosi akifa basi na nyie mliobaki ndio mshindwe vita?.
Kushindwa kwa upinzani inaweza kuwa ni alama moja wapo inayoonyesha kushindwa kwake maana kumbe hakujenga misingi ili yeye asipokuwepo mambo yaendelee bila shida, kifupi alikuwa mbinafsi.
Kama kweli aliamini kwenye upinzani na alituaminisha alichotuaminisha alikuwa na sababu gani ya kurudi CCM na sio kuanzisha chama chake ili aendeleze falsafa na misingi yake kwenye harakati za kukomboa tanzania?
 
Kalewa Kwa nini wanatumia polisi kuzuia chama kuzungumza na wanainchi anashindwa mchana kweupe
 
Lowasa alivokatwa kijani kibichi nilishangilia sana lakini nilifubazwa na Chama changu kumkaribisha, kama alivofanya Slaa ni bora ata nngekua mm nngefanya chochote si kukubali Yule mzee aende Ikulu........

Angeenda Ikulu ninnngeishangaa sana hii Tanzania yangu.....
 
Mbona yeye alikuwa na ajenda na bado akashindwa kumtoa JK mwaka 2010. Ameshindwa kuujua ukweli kuwa vyombo vya maamuzi vyote vipo chani ya chama dola.

Halafu huyu si alishaapa kuwa atakuwa mwaminifu kwa rais? Huyu boss wake si ni Augustine Mahiga ambaye boss wake ni Magufuli? Yani yupo chini ya boss mmoja kumfikia boss wake na bado analeta maneno mengi.
 
Hiki kibanu kinalinda ajira yake hakina lolote.

Baaada ya kutoka CHADEMA alidhani chama kingekufa ila sasa anaona hali ni tofauti hivyo roho inamuuma.

Sharito mojawapo lisilotamkwa rasimi hadharani la wateule wa awamu hii kupanda vyeo,kulinda vyeo na hata kupata uteuzi, ni kushambulia upinzani, kuhujumu upinzani na kujipendekeza kwa boss wao kwa kumuimbia mapambio na kumsifu na wala sio utendaji mzuri wa kazi.
Ukweli tusiotaka kuukubali ni kuwa CHADEMA imeshajifia hadi sasa, na ukitaka kuthibitisha hili subiri 2020, chama kimeshindwa kushawishi wanachama wake kuwa na utayari wa kukipigania chama kwa jasho, machozi na damu kama kilivyokua wakati Dr. Slaa yupo. Sa hivi viongozi wanaweza kuambiwa wanachama wao wamekamwatwa wako police na wasijali chochote kile. Hata vyombo vya dola vimeshaanza kuwadharau sasa hivi kwa sababu hawana tena ile heshima waliyokuwa nayo.

Zamani Mbowe angeweza kusema sasa tunaingia barabarani kudai katiba mpya na Tanzania nzima ikaingia barabarani, ila sasa nani atamsikiliza? Toka Slaa aondoke chadema hakuna upinzani wowote chama kimeleta kwa CCM, Chaguzi zote zimekua sio za haki, lakini Chadema hawajafungua hata kesi moja ya uchaguzi, sasa utasema kuna upinzani hapo. Sometime hata wanaohama pamoja na ujinga wao wote ila siwalaumu, mana hata wakibaki hakuna wanachofanya zaidi ya kuendelea kuumia tu.
 
Kwa akili ya kawaida alitegemea sisi tutaamini kuwa atawezakuenda kinyume na matakwa ya Jiwe! Mpaka Kichefu chefu huu Utawala, waliipewa madaraka akili zao wameziweka Makalioni sasa!
 
Back
Top Bottom