Wilaya ya Sikonge hali ya Usalama ni ndogo. Serikali amkeni

Mnabuduhe

JF-Expert Member
May 8, 2015
352
590
Habari zilizonifikia leo Kuhusu yanayoendelea Wilayani Sikonge, Mkoani Tabora si ya kawaida kwa Nchi ambayo kuna Viongozi wa Serikali wanaolipwa Mshahara na Malupulupu Kibao.

Kesho jioni nitakuwa Wilayani Sikonge Kuleta ripoti Kamili ya Kiuchunguzi.

Kwa Mukhatasari tu! Matukio ya Watu Kuvamiwa na kuchinjwa kama Kuku yamekithiri wilayani humo kwa Miezi takribani minne sasa. Mpashaji wa habari hizi ananialifu kuwa majuma matatu yaliyopita katika Mtaa wa Majengo Wilayani Sikonge Mnamo majira ya Saa sita Usiku kuelekea saa Saba, Mama na Binti yake walivamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni Majambazi na kukatwa katwa mapanga.

Wahalifu hao walianza kwa kumshambulia Mama wa mji huo na ndipo binti akaingilia kumuokoa mama yake akaishia kuuwawa kikatili na kufia Katika Hospitali teule (Sikonge DDH) maarufu kama Hospitali ya Misheni mjini humo. Wakati Mama aliyenusurika na bado hata hajapona majeraha vema, Usiku wa kuamkia jana tarehe 12/12/2020 katika Mtaa huo huo wa Majengo jirani na OCD Mstaafu Mzee Edward Mturo Watu wawili walivamiwa na kukatwa mapanga na kufariki papo hapo.

Kijana aliyetambuliwa kwa Jina moja tu la Athanas Mwenyeji wa Wilaya ya Karatu aliyekuwa akijishughulisha na Biashara ya Kuuza Vinywaji na Maji Katika Stendi Ndogo ya Mabasi Mjini humo ameuawa Kikatili pamoja na Mkewe ambaye alikuwa Mjamzito hivyo kufanya Nafsi Tatu kupoteza maisha kwa siku Moja.

Mbali na Matukio haya yaliyotokea hivi Karibuni kama miezi miwili iliyopita mauji ya mtindo huo huo yalitokea katika Kijiji cha Mwanamkola nje kidogo ya mji wa Sikonge na katika Kijiji cha Chabutwa Wilayani humo.

Wananchi wamebakia na taharuki kubwa juu ya Usalama wa maisha yao,na wananchi wengi wanalitupia lawama jeshi la polisi kuwa wameshindwa kutimiza wajibu wao katika kuhakikisha kuwa wanaendelea kuwa Salama,ukizingatia mtaa ambao mauji ya hivi karibuni yametukia ni eneo ambalo Askari polisi wengi walinunua viwanja na kutengeneza makazi yao (na kupewa jina la mtaa wa line polisi).

Mh. Mkuu wa Wilaya hiyo Bwana Peresi Magiri hakupatikana mapema kutolea ufafanuzi wa matukio haya kama Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa Wilaya,wakati wananchi wa Wilaya hii wakitoa wito kwa Viongozi wa Ngazi za juu Kuimulika Sikonge kwa Jicho la Kipekee kwani Taswira yake na Amani yake imechafuka vibaya, hata wale waliokuwa wanadhani wanaweza kuja na kufanya Shughuli zao hapo hawawezi kufanya Hivyo.

Mkuu wa WIlaya, OCD Mwampamba pamoja Na DSO walifika katika Eneo la Tukio hilo jana Asubuhi mbali ya kuwa raia Wema na majirani walitoa taarifa mapema kabisa wakati walipoona hali ya Uvamizi inaendelea katika eneo hilo.

Ni bora Wakati wa Uongozi wa RC Aggrey Mwanri aliyependa sana kuitembelea Sikonge kila baada ya muda mfupi na kukemea kwa nguvu juu ya matukio ya namna hiyo.

Habari zaidi itafuatia baada ya Mwandishi wa Habari hizi kufika Sikonge na Kuhakiki na Kuleta ripoti ya Kina.
 
Fika kwanza mkuu unaweza kuwasaidia kupaza sauti maana "geshi letu la Polisi" sote twalijua linavyopambana kuweka mambo sawa, ila lingekuwa ni suala la kisiasa sipat picha
 
Washauri wenzako muweke ulinzi shirikishi aka sungusungu utakuja kutushukuru. Popote ilipoanzishwa sungusungu haijawahi kufeli.
 
Mkuu uwe Makini utakapo kuwa unafanya habari za kichunguzi maeneo hayo.

Rejea kupotea kwa Azzory Gwanda ,wana habari mnafanya kazi katika Mazingira magumu sana awamu hii.
 
Anzisheni matawi mengi ya Chadema mtaishi kwa amani, polisi watahamia huko na kila siku mazoezi mitaani.
Kama sikosei kituo cha kwanza cha polisi kujengwa huko ni baada ya Kasanga Tumbo kutofautiana na J. K. Nyerere.
 
Pole yao Sikonge uchunguzi wa haraka ufanyike kubaini chanzo cha haya matukio kabla Hali haijawa mbaya zaidi kamati ya ulinzi Wilaya imelala sana.
 
Ni kitendo cha muda, mji wa Tabora upo chini ya RPC nguli kabisa, nakumbuka kwa umahiri wake wa kufikiri kipindi anafundisha law enforcement Mlimani
 
Ni kitendo cha muda, mji wa Tabora upo chini ya RPC nguli kabisa, nakumbuka kwa umahiri wake wa kufikiri kipindi anafundisha law enforcement Mlimani
Chenga tu anafanya kazi theoretically azame field na vijana
 
Back
Top Bottom