Makirita Amani
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 1,914
- 3,440
Leo naona vijana wengi wakifurahia kwamba leo ni wikiendi ya hela.
Hii ni kwa sababu timu kubwa duniani zinacheza leo, hivyo kama wakibashiri vizuri matokeo ya michezo hiyo wanategemea kupata fedha nyingi kwa kuweka kidogo (BETTING)
Naomba niwakumbushe vijana wenzangu kwamba wikiendi ya fedha haipo hivyo. Kwa kila watu 10 watakaobet leo, mmoja pekee ndiye atakayeshinda, tisa watapoteza, yaani wataliwa. Lakini hawatakata tamaa kwa sababu wanamwangalia yule mmoja aliyeshinda na kuona ipo siku yao. Huku ni kujidanganya.
Mchezo wowote wa kamari, kama hizi beting, umetengenezwa kwa njia ya kwamba wachache washinde, ili kuwahamasisha wengine waendelee kucheza, lakini wengi waliwe, ili makampuni yanayoendesha kamari hizi yapate faida KUBWA.
Sasa rafiki sitaingia zaidi huko kwa leo, lengo langu ni kukuonesha wikiend halisi ya hela ikoje.
WIKIEND HALISI YA HELA IKO HIVI,
Unaamka asubuhi na mapema mno, kabla jua halijachomoza,
Unaipangilia siku yako, kwa kuandika malengo yako na mipango ya siku hiyo.
Unaondoka na kuwahi eneo lako la kazi au biashara, unaanza shughuli zako mapema kabisa.
Unaweka juhudi kubwa kuhakikisha unatoa thamani kubwa kwa wale wanaopokea unachofanya.
Hiyo sasa ndiyo wikiend ya hela, wikiend ya hela hasa, ambayo huwezi kuliwa.
Hivyo rafiki, nimalize kwa kusema kwamba;
Unaweza kuchagua kwenda kuongeza thamani leo, au unaweza kuchagua kwenda kuliwa hela zako leo, ni maisha yako, ni maamuzi yako, usije tu ukasema hukujua.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
www.makirita.info