Wiki ya mabingwa & tarehe ya Simba Day

Hadrianus

JF-Expert Member
Feb 19, 2020
691
1,000
UONGOZI wa Simba umesema kuwa kuanzia kesho Ijumaa, Agosti 14 utaanza kutambulisha wachezaji wapya ambao umemalizana nao kwa ajili ya msimu wa 2020/21 pamoja na kutambulisha uzi mpya watakaoutumia.

Miongoni mwa wachezaji wapya ambao wanatarajiwa kutambulishwa na Simba ni pamoja na Ibrahim Ame kutoka Coastal Union, David Kameta,'Duchu' kutoka Lipuli, Charlse Ilanfya kutoka KMC ambao wataungana na Bernard Morrison kutoka Yanga.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, leo Agosti 13 kwenye Ukumbi wa Hotel ya Serena, Manara amesema kuwa;"Kesho Ijumaa tutazindua nembo mpya ya klabu. Tumeiboresha ili iendane na soko la sasa. Baada ya uzinduzi wa logo mpya tutazindua jezi mpya ya Simba ya msimu na tunaanza kutanganza wachezaji wapya.

Pia Manara amesema kuwa Simba inaunga mkono jitihada za Serikali katika masuala yote ikiwa ni pamoja na masuala ya utalii hivyo amewaomba mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya utalii.

"Katika kuunga mkono Serikali, Jumatatu na Jumanne kupitia matawi yote nchi nzima. Wanasimba wote tutembelee vivutio vya utalii. Ni siku maalumu Wanasimba kuunga mkono utalii wa ndani." amesema.

Tarehe 22/08/2020 ndiyo itakua Simba Day
 

Noti bandia

JF-Expert Member
May 3, 2020
555
1,000
Badala ya kujiandaa na mashindano ya kimataifa endeleeni na mbwembwe nyingi afu mechi ya kwanza tu mnarudi kucheza na utopolo huku mchangani. Timu zetu hz zinahitaji maandalizi ya muda mrefu ili kuweza kushindana na timu kubwa huko.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom