Wiki moja ya kampeni Igunga

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,781
  • Thursday, September 15, 2011, 13:28
  • Habari, Rai

Mikataba mibovu ya madini yaitesa CCM *Wao wajivunia mtandao wa wanachama *CHADEMA walia na ugumu wa maisha *CUF wajivunia mtaji wa kura 11,000

Na Waandishi Wetu, Igunga

WIKI moja tangu kuanza mchakamchaka wa kampeni za ubunge katika Jimbo la Igunga mkoani Tabora, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) sasa vinatoana jasho.

Kampeni za CCM ambazo zilizinduliwa Jumamosi iliyopita na Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, zinaendelea kwa kuhusisha viongozi mbalimbali wa kitaifa wakiwamo mawaziri.

Kwa upande wa CHADEMA, tangu kuanza kampeni zake wiki iliyopita, zimekuwa zikiongozwa na Katibu Mkuu wake, Dk. Wilbroad Slaa, akisaidiana na baadhi ya wabunge na viongozi wengine wa chama hicho.

CCM katika mikutano yake, wamekuwa wakimnadi mgombea wao Dk. Peter Kafumu, kwa kutumia karata ya kiwango chake cha elimu na historia yake katika utumishi wa umma.
Katika mikutano yake ya kampeni, wamekuwa wakijivunia maendeleo yaliyopatikana nchini katika kipindi cha miaka 50 tangu kupatikana kwa Uhuru.

Pia katika kile kinachoonekana kupanda kwa joto la kampeni, chama hicho kimekuwa kikidai wapinzani wao wakuu, CHADEMA, si watu wa kuaminiwa pamoja na kuwahusisha na baadhi ya matukio ya vurugu katika mchuano huo.

Kwa upande wao CHADEMA, wametumia wiki ya kwanza ya kampeni kuhakikisha sera zao zinawafikia wananchi wote hata wale wa vijijini, ili mgombea wao, Mwalimu Joseph Kashindye, ashinde kwenye uchaguzi huo.

Katika mikutano ya kampeni, chama hicho kimekuwa kikiwanyoshea vidole CCM kwa kushindwa kuwaondolea umasikini Watanzania na wananchi wa Igunga kwa ujumla.
Miongoni mwa hoja zinazotumika ni pamoja na tatizo la kupanda bei kwa bidhaa muhimu kama chakula, mafuta, kushuka kwa thamani ya shilingi, uduni katika huduma za afya, maji na suala zima la ubovu wa miundombinu ya barabara.

"CHADEMA wanapopanda jukwani na kujenga hoja, unaona uhalisia wa mambo, hawa wanazungumzia matatizo ya msingi ya wananchi, hasa umasikini ambao unawatesa.
"Tukumbuke kuwa walitoa elimu ya uraia kabla ya kuanza kwa kampeni, kwa hiyo hii nayo inawasaidia, kwa sababu hata watu wa vijijini sasa wameanza kuelewa ni nini maana ya upinzani, na vigumu kuwadanganya kamailivyokuwa zamani," alisema mkazi mmoja wa Igunga, ambaye ni mtumishi wa Halmashauri.

Pia katika kampeni hizo, vyama vya upinzani vimekuwa vikimtuhumu Dk. Kafumu wa CCM kwamba wakati wa Rais benjamin Mkapa, akiwa Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini, alishiriki moja kwa moja katika mchakato wa kuandaa mikataba mibovu ambayo imeingiza nchi hasara kubwa. Mikataba ya Madini inalalamikiwa kwa kutowanufaisha wananchi.

Chama cha Wananchi (CUF), chenyewe kilifanya uzinduzi wa kampeni Jumanne wiki, na Mwenyekiti wake Taifa, Profesa Ibrahim.

Pamoja na mambo mengine, Profesa Lipumba aliwataka wananchi wa Igunga kutompigia kura mgombea wa CCM, na badala yake wamchague mgombea wa chama hicho, Lepold Mahona, kwa kuwa CCM kimepoteza mwelekeo na kimeshindwa kuwaletea maendeleo Watanzania.

Kwa pamoja vyama vyote vitatu vimefanya uzinduzi wa kampeni zao katika Uwanja wa Sokoine uliopo mjini hapa, kutokana na ukaribu na eneo husika ulipo na maeneo ya biashara na makazi ya watu wa mji wa Igunga.

Tangu kuzinduliwa kwa kampeni mjini hapa, hali ya utulivu na kampeni za kistaarabu imekuwa ikisisitizwa na kila mwanasiasa au mdau anayesimama kuzungumzia kampeni za Igunga.

Wachambuzi wa mambo mjini hapa wanasema msisitizo huo unatokana na hali halisi ya utamaduni na asili ya wananchi wa Igunga, ambao ni watu wenye kupenda amani na utulivu.

Hali hiyo ilijidhihirisha wakati CHADEMA na CUF walipokuwa wakirudisha fomu kwa Msimamizi wa Uchaguzi, ambapo vyama hivyo vilijikuta wafuasia wake wakigongana kwenye njia na kusababisha tafrani kidogo.

Hata hivyo, aina ya watu ambao walionyesha majibizano na hata kutaka kuonyesha ubavu wa siasa za vurugu, hawakuwa wananchi wenye asili ya Igunga, bali walikuwa ni wageni waliokuja kwa ajili ya kampeni za vyama vyao.

Akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa vilivyoweka wagombea, Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi, Kitengo cha Oparesheni, Issaya Mngullua, alisema kila mtu aliyepo Igunga anawajibu wa kulinda amani iliyopo.

"Ndugu zangu uchaguzi utaisha na Igunga itabakia na shughuli zake, hivyo nawaomba tuhakikishe unafanyika uchaguzi wa amani na utulivu.

"Askari polisi wapo, japo hawawezi kutosha kwa maana ya kulinda kila kona ya mji au kulinda bendera na mabango ya wagombea yasichanwe, hili ni gumu kwetu.

Nategemea kila mtu akitimiza wajibu wake hali ya amani itakuwapo," alisema.

Kwa upande wake, Mjumbe Baraza Kuu la Uongozi Taifa CUF, Mhina Omari, alisema kama vyombo vya dola vitatenda haki katika kusimamia uchaguzi wa Igunga, hakuna chama kitakachokuwa na jeuri ya kuanzisha fujo.

Alisema jambo la msingi ambalo Msimamizi wa Uchaguzi anapaswa kulifanyia kazi kwa umakini, ni siku ya kutangaza matokeo, kwani ndipo huanzia dalili zote za vurugu.

"Tusingependa kuona msimamizi siku hiyo akijizungusha kutangaza matokeo, hili ni jimbo moja, siku hiyo licha ya msimamizi kuwa na matokeo hata sisi tutakuwa nayo, ila tu hatutaweza kuyatangaza," anasema Omari.
 
nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,781
  • Thursday, September 15, 2011, 13:28
  • Habari, Rai
Na Waandishi Wetu, Igunga

Mikataba mibovu ya madini yaitesa CCM *Wao wajivunia mtandao wa wanachama *CHADEMA walia na ugumu wa maisha *CUF wajivunia mtaji wa kura 11,000

WIKI moja tangu kuanza mchakamchaka wa kampeni za ubunge katika Jimbo la Igunga mkoani Tabora, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) sasa vinatoana jasho.Kampeni za CCM ambazo zilizinduliwa Jumamosi iliyopita na Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, zinaendelea kwa kuhusisha viongozi mbalimbali wa kitaifa wakiwamo mawaziri.

Kwa upande wa CHADEMA, tangu kuanza kampeni zake wiki iliyopita, zimekuwa zikiongozwa na Katibu Mkuu wake, Dk. Wilbroad Slaa, akisaidiana na baadhi ya wabunge na viongozi wengine wa chama hicho.

CCM katika mikutano yake, wamekuwa wakimnadi mgombea wao Dk. Peter Kafumu, kwa kutumia karata ya kiwango chake cha elimu na historia yake katika utumishi wa umma.

Katika mikutano yake ya kampeni, wamekuwa wakijivunia maendeleo yaliyopatikana nchini katika kipindi cha miaka 50 tangu kupatikana kwa Uhuru.

Pia katika kile kinachoonekana kupanda kwa joto la kampeni, chama hicho kimekuwa kikidai wapinzani wao wakuu, CHADEMA, si watu wa kuaminiwa pamoja na kuwahusisha na baadhi ya matukio ya vurugu katika mchuano huo.

Kwa upande wao CHADEMA, wametumia wiki ya kwanza ya kampeni kuhakikisha sera zao zinawafikia wananchi wote hata wale wa vijijini, ili mgombea wao, Mwalimu Joseph Kashindye, ashinde kwenye uchaguzi huo.

Katika mikutano ya kampeni, chama hicho kimekuwa kikiwanyoshea vidole CCM kwa kushindwa kuwaondolea umasikini Watanzania na wananchi wa Igunga kwa ujumla.
Miongoni mwa hoja zinazotumika ni pamoja na tatizo la kupanda bei kwa bidhaa muhimu kama chakula, mafuta, kushuka kwa thamani ya shilingi, uduni katika huduma za afya, maji na suala zima la ubovu wa miundombinu ya barabara.

“CHADEMA wanapopanda jukwani na kujenga hoja, unaona uhalisia wa mambo, hawa wanazungumzia matatizo ya msingi ya wananchi, hasa umasikini ambao unawatesa.
“Tukumbuke kuwa walitoa elimu ya uraia kabla ya kuanza kwa kampeni, kwa hiyo hii nayo inawasaidia, kwa sababu hata watu wa vijijini sasa wameanza kuelewa ni nini maana ya upinzani, na vigumu kuwadanganya kamailivyokuwa zamani,” alisema mkazi mmoja wa Igunga, ambaye ni mtumishi wa Halmashauri.

Pia katika kampeni hizo, vyama vya upinzani vimekuwa vikimtuhumu Dk. Kafumu wa CCM kwamba wakati wa Rais benjamin Mkapa, akiwa Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini, alishiriki moja kwa moja katika mchakato wa kuandaa mikataba mibovu ambayo imeingiza nchi hasara kubwa. Mikataba ya Madini inalalamikiwa kwa kutowanufaisha wananchi.

Chama cha Wananchi (CUF), chenyewe kilifanya uzinduzi wa kampeni Jumanne wiki, na Mwenyekiti wake Taifa, Profesa Ibrahim.

Pamoja na mambo mengine, Profesa Lipumba aliwataka wananchi wa Igunga kutompigia kura mgombea wa CCM, na badala yake wamchague mgombea wa chama hicho, Lepold Mahona, kwa kuwa CCM kimepoteza mwelekeo na kimeshindwa kuwaletea maendeleo Watanzania.

Kwa pamoja vyama vyote vitatu vimefanya uzinduzi wa kampeni zao katika Uwanja wa Sokoine uliopo mjini hapa, kutokana na ukaribu na eneo husika ulipo na maeneo ya biashara na makazi ya watu wa mji wa Igunga.

Tangu kuzinduliwa kwa kampeni mjini hapa, hali ya utulivu na kampeni za kistaarabu imekuwa ikisisitizwa na kila mwanasiasa au mdau anayesimama kuzungumzia kampeni za Igunga.

Wachambuzi wa mambo mjini hapa wanasema msisitizo huo unatokana na hali halisi ya utamaduni na asili ya wananchi wa Igunga, ambao ni watu wenye kupenda amani na utulivu.

Hali hiyo ilijidhihirisha wakati CHADEMA na CUF walipokuwa wakirudisha fomu kwa Msimamizi wa Uchaguzi, ambapo vyama hivyo vilijikuta wafuasia wake wakigongana kwenye njia na kusababisha tafrani kidogo.

Hata hivyo, aina ya watu ambao walionyesha majibizano na hata kutaka kuonyesha ubavu wa siasa za vurugu, hawakuwa wananchi wenye asili ya Igunga, bali walikuwa ni wageni waliokuja kwa ajili ya kampeni za vyama vyao.

Akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa vilivyoweka wagombea, Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi, Kitengo cha Oparesheni, Issaya Mngullua, alisema kila mtu aliyepo Igunga anawajibu wa kulinda amani iliyopo.

“Ndugu zangu uchaguzi utaisha na Igunga itabakia na shughuli zake, hivyo nawaomba tuhakikishe unafanyika uchaguzi wa amani na utulivu.

“Askari polisi wapo, japo hawawezi kutosha kwa maana ya kulinda kila kona ya mji au kulinda bendera na mabango ya wagombea yasichanwe, hili ni gumu kwetu. Nategemea kila mtu akitimiza wajibu wake hali ya amani itakuwapo,” alisema.

Kwa upande wake, Mjumbe Baraza Kuu la Uongozi Taifa CUF, Mhina Omari, alisema kama vyombo vya dola vitatenda haki katika kusimamia uchaguzi wa Igunga, hakuna chama kitakachokuwa na jeuri ya kuanzisha fujo.

Alisema jambo la msingi ambalo Msimamizi wa Uchaguzi anapaswa kulifanyia kazi kwa umakini, ni siku ya kutangaza matokeo, kwani ndipo huanzia dalili zote za vurugu.

“Tusingependa kuona msimamizi siku hiyo akijizungusha kutangaza matokeo, hili ni jimbo moja, siku hiyo licha ya msimamizi kuwa na matokeo hata sisi tutakuwa nayo, ila tu hatutaweza kuyatangaza,” anasema Omari. 

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,504
chadema shikilieni uzi huo huo achanane na mkapa endeleeni kukazia kamba kwenye kitu wazungu wanaita kitchen table issues maji, umeme, barabara, shule, ajira, bei ya vyakula, mafuta ya taa, sukari na kadhalika kwani ktk maeneo hayo CCM haina cha kuwaambia wananchi kwani wenyewe wanayaona.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom