wiki la CDA Dodoma : Mamlaka imefanya kazi gani mpaka sasa?

minda

JF-Expert Member
Oct 2, 2009
1,068
65
wakuu,
mamlaka ya ustawishaji makao makuu dodoma, CDA, lililoanzishwa kwa notisi namba 230 ya serikali ya tanzania ya tarehe 12 desemba, 1973; juma hili linasherehekea wiki lake kwenye viwanja maarufu vya nyerere square mjini dodoma, na kaulimbiu ni:

wiki la cda: tujenge mji kwa pamoja

mengi yameandikwa kwenye tovuti ya cda kuhusu kazi za mamlaka hayo, lakini mpaka leo hii, miaka 37 tangu maamuzi kufanyika kuhusu mji huu wa chifu mazengo(tamka: madzengo) na mkewe masalatu(sio msalato!), kuwa makao makuu ya tanzania bado utekelezaji wake haujakaa sawa.



ukimuuliza mkazi wa kawaida wa dodoma kuhusu cda utapata maneno haya:
  • bomoa bomoa
  • rushwa (kigogo wake amefukuzwa kazi na utumishi miezi kadhaa iliyopita)
  • ulaji wa madalali
  • una ndugu kupata kiwanja cha kupimiwa na dodoma?
  • wafanyakazi wake mamilionea
  • kiwanja sipati labda ninunue 'shamba'
  • mji mdogo wa 'maisha plus' nkuhungu
  • chang'ombe/gwasa
  • yaliyotokea mjedengwa kwa bilingi?
  • image kwa wakubwa na matajiri
  • ongezea
kama tathmini kuhusu kazi zake kama nilivyoorodhesha hapo juu, naweza kusema kwamba wakaazi wa dodoma na watanzania kwa ujumla wana 'malalamiko' kuhusu kasi ya upimaji viwanja unaogubikwa na 'usiri' wa hali ya juu na maendeleo ya dodoma itakayokuwa makao makuu ya nchi, kama cda itafanikiwa kuuendeleza.

my ake:



1. wakuu mnasemaje kuhusu;
  • kasi ya upimaji wa viwanja kwa wakazi wa dodoma?
  • kasi ya ukuaji wa mji kutokana na kazi za cda kutakakopelekea mji wa dodoma kufanywa kuwa makao makuu ya tanzania?
2. karibuni kwenye viwanja vya nyerere square ili kupata habari mbalimbali kuhusu mamlaka hayo kutoka kwa wahusika wenyewe.

naomba kuwasilisha!!!
 
Back
Top Bottom