Che Kalizozele
JF-Expert Member
- Jul 20, 2008
- 777
- 49
hahahaha nashukuru sana baba mkwe Che,
mi nipo single natafuta bado nashukuru kwa mikono miwili hii ofa nono ahsante sana naipokea tena kwa mikono miwili........naomba unikabidi mwali kabisaaaaaa mapema baba mkwe.
Unajua uwa unanifurahisha sana,nitakupa mwanangu mmoja uoe,kama haujaoa lakini.Mahari yako ni kunichekesha baba mkwe wako siku nzima.
Masikini wee, laiti baba mkwe mtarajiwa angekujua ulivyo!..Anyway tusikuharibie bahati yako, hongera na umtunze vizuri mwali kama utapewa lakini!..ha ha ha
Ah ina maana mwenzetu huyu atakuwa analipa mahari siku zote za uhai wake?... kaaaaaazi kwerikweri.
Haya Fidel tengua udhu haraka sana. Bado nipo nipo haikufai tena wazeeka sasa ona hizo ndevu zishakuwa na mvi sasa kaka (Joke)
Hivi Belinda nitakuwa nina kichaa cha kiasi gani mpaka nikamtupe mwanangu kwa fidel.Hata siwezi kujaribu.
Haya Fidel tengua udhu haraka sana. Bado nipo nipo haikufai tena wazeeka sasa ona hizo ndevu zishakuwa na mvi sasa kaka (Joke)
Watu bana tayari wamesha haribu ridhiki....anyway ridhiki ya Simba ipo miguuni mwake...baba mkwe wasikukatishe tamaa hawa wana wivu tu.
teh teh teh mi nachekelea tu utafikiri ndo nyie mnao ninyima hata ofa ya maji ya kunywa tu mniache Kitonga....hii tayari yangu,
Yaani kama nakuona na suruali yako ya kifua, ulimi umekutoka mpaka kidevuni kwa uchu. Mtoto wa watu bado mdogo (tena wa bara huyo) usimharibu.
Karibu,lakini si umesema umeshaoa japo upo upo,ukimaanisha your ndoa is not working.Labda umuache kwanza huyo ndo umuoe mwanangu,bado mdogo si wakupata frustration mapema kiasi hiki ya uke wenza.
Mimi ni mdada mtu mzima tu nimeolewa miaka si chini ya mitano, nina watoto wawili. Nimekuwa nikishindana na wifi yangu ambae ni dada wa damu wa mume wangu, ushindani wetu ni kama mtu na mke mwenzie lakini si hivyo.
Kabla sijaolewa na huyu mwanaume tulikuwa kwenye uhusiano wa mbali kwani mimi nilikuwa nasoma Ireland na yeye alikuwa Tanzania. Kipindi chote hicho hakukuwa na matatizo yeyote kati yangu na dada yake.
Baada ya kumaliza masomo nilihamia England kufanya kazi ambako ndiko tunaishi mpaka sasa. Ndoa yetu ilifungiwa Tanzania na Mume wangu akanifuata huku na baada ya muda tukasaidiana na kumleta dada yake ambaye ndio wifi yangu huyu mwenye vituko kila kukicha ambavyo vinahatarisha ndoa yangu.
Imefikia hatua wifi yangu kuchagua nini kifanyike ndani ya nyumba yangu, aina gani ya vifaa vinunuliwe ikiwa tunafanya marekebisho hapa ndani, wapi tuende au tusiende, tukamtembele nani nalini na kinachonikasirisha zaidi ni kaka mtu kumsikiliza dadake na sio mimi mkewe.
Ikitokea mimi na mume wangu tumejadili jambo la kufanya kwa ajili ya familia yetu ndogo mume wangu anachukua simu na kumwambie kila kitu mdogo wake na kitakachosemwa na mdogo wake basi ndio kitakachofanywa na sio mimi hata kama sehemu ya jambo hilo pesa zangu zinahusika. Yaani imekuwa kama akili ya mume wangu haifanyi kazi basi anatumia ya dada yake kufanya maamuzi.
Kitu kingine kinachoniumiza roho na kunipa donge ni pale ninapotoka kazini jioni au siku za mwisho wa wiki wote tuko nyumbani, badala mume wangu atumie muda huo na mimi yeye atakuwa kwenye simu na dada yake wakiongea maongezi yasiyoisha tena kwa kilugha chao na kucheka.
Nimevumilia sana na nimefanya vikao na ndugu wa pande zote mbili na hata kuzungumza na mume wangu lakini hakuna mabadiliko yeyote, nimekuwa mkiwa ndani ya ndoa yangu na sijui nini cha kufanya, japokuwa nampenda mume wangu lakini kama suluhisho ni kutoka kwenye hii ndoa basi nitatoka ili kutafuta amani na furaha kwingine lakini sio ndani ya ndoa hii.
"
Wifi yangu huyu ni mkubwa zaidi ya mume wangu, ameolewa na anawatoto kadhaa wote wako Mkoani Kagera Tanzania.
Naombeni ushauri ndugu zangu"
Ikitokea mimi na mume wangu tumejadili jambo la kufanya kwa ajili ya familia yetu ndogo mume wangu anachukua simu na kumwambie kila kitu mdogo wake na kitakachosemwa na mdogo wake basi ndio kitakachofanywa na sio mimi hata kama sehemu ya jambo hilo pesa zangu zinahusika. Yaani imekuwa kama akili ya mume wangu haifanyi kazi basi anatumia ya dada yake kufanya maamuzi.
Kitu kingine kinachoniumiza roho na kunipa donge ni pale ninapotoka kazini jioni au siku za mwisho wa wiki wote tuko nyumbani, badala mume wangu atumie muda huo na mimi yeye atakuwa kwenye simu na dada yake wakiongea maongezi yasiyoisha tena kwa kilugha chao na kucheka.
Duuh..ebwanaeeeeeheheeee...sikiza bibie...mbona unaonekana UMEMUOA huyo fa--r--a lakini hutumii nguvu yako ya VETO ya "kumwoa" na kumpa masharti magumu kama hayawezi achape mwendo arudi kijijini akalime mwani...kama nitakuwa nimekosea naomba unisahihishe...ulikuwa unasoma abroad ukaja tzania mkafunga ndoa kisha ukaondoka naye huyo mmeo...then nakonkludi kuwa ULIKUJA KUMWOA NA KUONDOKA NAYE KUMHAMISHIA NYUMBANI KWAKO...ndio..kama angekuwa kakuoa angekaa na wewe kwake i.e tzania....unayo haki ya msingi ya kumwambia achague moja..dadake au wewe "mme wake"...kuhusu ukionacho wewe ni tatizo..WIFI YAKO...huyo naye mie naona mbona mwepesi tuuu...mtafutie ticket achape mwende mpaka kagera akalee wanawe na mmewe pia...aache ungese wa kukaa kwenye nyumba za watu na kuingilia mambo yao...natumai kama vile hapungui 45yrs na bado anakaa kwenu?..thats a shame....hii nayo ni nyingine na ni kwa taarifa yako....hawa ndugu zetu wa kagera wanamambo yao (wengi wao na sio wote..na pia nisamehewe kwa kuweka ukwseli huu)....naamini huyu wifi yako ameshakuwa-swahiba wa kaka yake katika kumtafutia totozi hasa hizi za jamii ya kagera pia...ndoa ya wakagera huwa inaenda vizuri wakiwa wao-kwa - wao ndio wahusika...sasa wewe dada yangu intruder wa mila za watu naona umegeuzwa buzwagi..wanakula shavu ....kama unakifua wamwage wote..naona kama wanakuwa mzigo kwako mara 2...kiuchumi...unahangaika wanakula na kulala...then wanakutesa kwa mambo yao ya kipuuzi.......wanaume wapo kibaooo tu...single parent familiez kibaoooo tuu na HAPPY LIFE GOES ON
Mkuu
napenda tu kukutaarifu kwamba mie (kama si wengi humu) nashindwa kusoma posti zako kwa kuwa zipo zigzag mno. unachanganya sana rangi, bold, caps n.k.
pls shekhe kuwa mpole ktk hilo basi