So you treat life like a problem.
Something to fix?
Something to get right?
And so everything become seriously 😅
This is a logical non sequitur fallacy.
These are facts. Tumeona kwa macho. Tena kwetu si mbali.
Ukiishi leo kama hakuna kesho, hujajipanga na kesho, halafu kesho ikafika, hujajipanga kuikabili, utaumia.
Tuanze na mifano midogo tu kwenye familia zetu.
Mimi baba yangu kajenga nyumba mbili Mbezi Beach na moja Mwanza, akiwa kijana kaanza miaka ya early 1980s huko , alikuwa ananunua mashamba Mbezi ya Morogoro Road mwaka 1992, bei chee, kwa laki laki, kanunua mashamba 15.
Leo Mbezi Beach hapashikiki. Huwezi kujenga kwa urahisi kama walivyojenga hawa wazee waliowahi. Kununua kiwanja tu no ndoto kwa wengi.
Tena yeye alikuwa anajilaumu angewahi kidogo angeweza kujenga viwanja fulani vya Msasani/Masaki kule.
Hayo mashamba ya Mbezi ya Morogoro Road ndiko ukioita kidogo wamejenga kituo cha manasi cha Magufuli sasa hivi. Shamba moja unaweza kukuta milioni 80 au zaidi.
Sasa hivi Mzee yupo comfortable tu ana mashamba yake all over, ana nyumba zake all over, analipwa rent in USD. Anaamua tu sasa hivi naenda kuangalia shamba langu Iringa au naenda kuwaangalia watoto wangu na wajukuu zangu USA. Anaendesha ndinga za uhakika, matibabu anakuja kupata USA, kajiandaa vizuri na maisha ya uzeeni.
Angeishi kama kesho haipo angejirusha tu, angekuwa anapigika sana sasa hivi anaishi kwa kujitegemea, hategemei watu wamsaidie.
Huelewi wapi?