Hili suala zaidi ni psychological. Watu tunapenda kupendwa, tena ikiwezekana tupendwe sana. Lakini shida kupendwa sana mara hugeuka kuwa kama kero vile, huchosha na kukinai. Mtu anaanza kujiskia kama mtumwa vile, kama yuko gerezani vile kwa sababu ya 'kukamatwa' na mtu. Kumbe kinachofuata mtu anaanza kujinasua, kutafuta uhuru kutoka gereza hilo.
Kwa kifupi watu hupenda mtu wa kufukuzia, yule anakupa shida kidogo, anayeonesha dalili - hata kama si za kweli - za kukuacha, yule anayeringa kidogo. Huyu hupendwa sana na kuvuta hisia za mpendwa wake. Na mara nyingi huyu mwenye maringo akishagundua wewe unamgwaya, naye hupenda kutafuta mwingine mwenye kumtesa moyoni mwake. Mi nadhani ndiyo maana ni ngumu sana kukuta watu wanaopendana sana sawia. Wapo lakini ni wachache