Why Me? (Kwanini mimi?)

Daniel Mtambo

Member
Mar 5, 2019
6
4
Kwanini Mimi
Mtunzi : Daniel John Mtambo

SEHEMU YA KWANZA (I)
Kila Jambo linalokukuta ktk maisha Ni makusudi ya Mungu.

Kijana Moja Aliyeitwa Aizaki John alikua Na elimu ya uhasibu ngazi ya degree, kwa mda wa miaka mwili toka alipohitimu elimu yake ya chuo kikuu, alizunguka sehem mbalimbali kutafuta kazi bila mafanikio, lakini siku moja alipigiwa simu Na mtu aliyejitambulisha kuwa Ni mwalimu mkuu wa moja kati ya shule alizowahi kuomba kazi Na kumjulisha kuwa kuna nafasi ya kazi ya uhasibu, alifurahi Na kumshukuru Mungu sana, kwakua alitakiwa kuripoti kesho yake alifanya maandalizi ya kwenda kuanza kazi,

****************

Kiufupi maisha ya Aizaki yalikua magumu sana kwakua hata Masomo yake yote aliweza kusoma kwa misaada mbalimbali ikiwemo michango ya waumini pamoja Na shirika la kusaidia watoto wanaoishi katka mazingira magumu.
Aizaki alifiwa Na mama yake tangu akiwa na umri wa miaka 12 baada yakifo cha mama yake, baba yake alioa mwanamke mwingine ambaye hakuwa na mapenzi kwa motto huyo aliyemkuta ktk ndoa, alimtesa sana hata hivyo kwakua baba yake Aizaki alimpenda sana mkwe huyo kiasi ambacho hakutaka kusikiliza malalamiko ya mtoto wake, Aizaki aliondoka nyumbani hapo Na kwenda kuishi na Bibi yake kijijini, Aizaki aliendelea na masomo na hatimae alihitimu masomo ya kidato cha sita, Aizaki alikua na bidii sana katika masomo pamoja na changamoto mbalimbali za ugumu wa maisha, hata hivyo alifanya vizuri sana ktk mtiani wake wa mwisho na alipofauru kwenda chuo kikuu alifunga safari kwenda kumjulisha baba yake ili amsaidie ada Na gharama za masomo, baba yake hakutaka kabisa kuonana na mwanae Na alipoona anapigiwa simu mara kwa mara aliamua kumblaklist. Kiufupi hakupata msaada wowote toka kwa baba yake mzazi, Hali hiyo ilimfanya kuwa anyonge sana Na mwwnyewe mawazo mengi kwakua aliamini baada ya kifo cha mama Ni baba yake pekee ndie angeweza kumfariji, lakini mambo yalikua tofauti Na mategemeo yake.

***************

Aliamka asubuhi Na mapema Na kwenda kuanza kazi ktk shule hiyo akiwa kama muhasibu, kazi zilienda vizur kabisa kiasi ambacho hata mwajili wake alifurahia uwezo aliokuwanao nao katka utendaji wakazi.


Aki wa ametimiza miezi mitatu tu ktk kazi yake, siku hiyo ulikua siku ya kufunga shule baada yakumaliza kazi yake aliitwa Na mkuu wake wa kazi, Na kupewa barua, kwakua hakujua kilichoandikwa aliiweka ktk begi lake nakuondoka ili akifika nyumbani aweze kusoma kwa utulivu, hatimae alifikanyumbani alifungua haraka barua ajue nini kiliandikwa ndani yake.

“ Mkuu Wa Shule, Yah: Kusitisha Mkataba wa Kazi yako ya Uhasibu
Ndg, Husika na Kichwa cha somo kama kinavyoeleza nianze kwa kuomba Samahani sana kwa hiki nitakachokueleza najua huwezi kukipokea lakini huna budi kukipokea kama kilivyoandikwa, tumepata malalamiko kutoka kwa baba yako mzazi kuwa Ni kwanini tumekuajiri wewe? Ameeleza kila kitu Na hakutuficha suala lolote kwamba umekimbia toka Arusha kwa kosa kutaka kumbaka mama yako mdogo. Pia umekua ukijihusisha Na madawa ya kulevya,hivyo kamati na bodi ya shule tumeamua kukusimamisha kazi ili kuepusha matatizo ktk shule yetu. Nyuma ya Hii barua ameambatanisha picha yako inayothibitisha kuwa kweli ulitaka kufanya tukio la ubakaji,
Naomba kama kuna kitu umekiacha hapa ofisini uje uchukue Na kuanza leo tafadhali usikanyage tena hapa shuleni.

Wako katika ujenzi wa Taifa
Mkuu wa Shule.

Aizaki alisoma barua hiyo mara tano kana kwamba lugha iliyoandikwa humo hakuielewa..
alishindwa kujua nini afanye kwa wakati ule zaidi alichokumbuka tu ni tukio ambalo lilitokea akiwa nyumbani kwa baba yake, ……Aizaki alikua ameenda kumsalimu baba yake wakati wa rikizo, mara nyingi baba yake alikua kazini hivyo nyumbani walibaki Aizaki na mama yake tu, Lakini Mama yake alikua ameingiwa na roho ya kumpenda sana Aizaki na kutaka afanye naye mapenzi, Siku hiyo mama yake huyo yake alimtaka kufanya naye mapenzi na baada ya Aizaki kukataa kufanya jambo hilo mama alimvizia Aizaki akiwa amotoka kuoga na akiwa amejifunga taulo, alipoingia tu chumbani kabla hajafunga mlango, mama huyo aliingia kwa ghafla na kumshika kwa nguvu akimbembeleza ili aweze kulala naye, wakati Aizaki akijaribu kujitoa mikononi mwa mama yake huyo ghafla akaona mwanga wa simu iliyokuwa imeshikwa na mama huyo, ishara tosha kuwa ilikuwa imepigwa picha, mama huyo alizidi kumforce Aizaki ili atomize haja zake lakini ilikuwa ni vigumu kwa kijana huyo kukubaliana na jambo hilo, mama huyo alijaribu kumweleza Aizaki kuwa endapo atakataa kufanya naye mapenzi basi angemwonesha baba yake picha hizo kuwa alikua anakusudia kumbaka, hali hiyo ilimpa wakati mgumu sana Aizaki na ndipo alipoamua kuondoka na kurudi nyumbani kwa bibi yake kabla hata rikizo haijaisha.,
Aliwaza mambo mengi sana lkn mwisho aliamua kumshukuru Mungu na Kusema kuwa, Asante Mungu kwakua hakuna jambo linaloweza kutokea pasipo wewe kuruhusu litokee.


Aizaki aliamua kurudi kijiji kwa bibi ake nakuamua kufanya kazi ya kilimo, Siku moja akiwa shambani Asubuhi akifyeka msitu mkubwa, alipita kijana mmoja na kumtania kwa kusema vipi Msomi, naona elimu ya chuo umeamua kuihamishia shambani....
Aizaki alijua kuwa ni kejeri hivyo alichukulia tu kama utani naye akajibu ...... Elimu sio lazima itumike ofisini kaka hata shambani inafaa pia.
Lakini kijana huyo aliondoka kwa kumsisitiza jambo, kuwa msitu huo ulikua na nyoka wakubwa pia walikua na sumu kali hivyo ni vema angeacha kazi hiyo au atafute eneo jingine,
Kwakua Aizaki alikua amedhamilia kuifanya kazi ile hivyo aliona ule ushauri ni kama kumkatisha tamaa,


dakika tano baada ya yule kijana kuondoka, akiwa ndani ya vichaka na zoezi lake la kufyeka, Aizaki alihisi kuna kitu kimemgonga begani kwa nguvu lakini alipogeuka hakuona kitu, na muda huo huo aliona uso unagubikwa na giza huku maumivu makali yakimuingia mwilini na kisha akaanguka nakupoteza fahamu.


Ilikua mida ya saa mbili usiku alisikia sauti za watu wakiongea kwa mbali, alipofumbua macho alikutana na watu asiowafahamu lakini aliweza kutambua kuwa mahali pale palikuwa ni Hospitali,


Aizaki unajiskiaje, alisikia sauti ikiuliza, sijambo ila naona maumivu tu ya kichwa kwani nimeumia? nani kanileta hapa, ninyi akina nani?
Aizaki aliuliza maswali kwa mfululizo, lakini mwishowe aliambiwa tulia pumzika kwanza, alikuuma nyoka, ukiwa shambani, ni sauti ya Nesi mmoja alisikika akimjibu.
Aliendelea kutibiwa hadi hali yake ikawa vema, siku iliyofuata alikuja daktari kumtembelea Akamuuliza Kijana hujambo, Aizaki Akajibu sijambo, pole sana uliumwa na nyoka mwenye sumu kali sana, endapo ungecheleweshwa kuletwa hapa ingekuwa tunazungumza habari nyingine, Unaishi nani,
Aizaki aliona aibu hata jinsi ya kujibu swali hilo kwakua aliona umri wake asingeeleweka kama ingejulikana anaishi kwa bibi yake, kabla hajajibu swali hilo machozi yalianza kumtoka na mwisho akashindwa kujizuia na kuanza kulia chini chini kiasi ambacho yule daktari alitambua kua kuna jambo flani ambalo limemsibu, hivyo alimwomba apumzike kisha atafika baadae kidogo kuja kumuona tena.....

*********************

Aizaki Alikua kijana mpole sana ambaye wakati mwingi hakupenda kuyaweka bayana maisha yake kwa kila mtu au kuelezea changamoto anazozipitia ktk maisha yake, alishindwa pia kumwamini mwanadamu yeyote, kwakua kila akikumbuka mkasa wa aliofanyiwa na rafiki yake wa karibu aliyesoma naye, ulimfanya awachukie watu wote, hata wale ambao walikua ni msaada kwake kuna wakati hakuwaamini.

Aizaki akiwa kidato cha kwanza katika shule moja ya sekondari kijijini kwao ndipo alipokutana na rafiki yake aliyeitwa Msafili. walikuwa wanatabia zinazoendana kwamaana hali ya kiuchumi kwao ilikua swawa walipofika kidato cha nne, kutokana na hali ngumu ya kimaisha aliyopitia Aizaki, Msafili alimwomba Mjomba wake wamchukue Aizack na kuishinae hapo kwa mjomba wake, hali ya mjomba wa Msafili kimaisha ilikua ni nzuri sana, Aizaki aliona kama amefungua ukurasa mpya ktk maisha yake wenye maisha ya furaha kwake, siku moja akiwa amelala usiku alisikia mlango unafunguliwa, kwakua lilikua giza kubwa hakuweza kuona nani aliyefungua mlango, Aizaki aliamua kupapasa pembeni yake ili Amwamshe Msafili Lakini akagundua kuwa pale kitandani alikua pekeake, mawazo yakamjia nakufikili kuwa Msafili atakua ametoka nje kwenda kujisaidia, lakini ghafla akakumbuka kuwa choo kiliwa ndani ya chumba chao, alistuka na kujikuta mapigo ya moyo yanamwenda mbio, aliamua kuita kwa sauti ya chini, Msafili..... msafili.... wakati anaendelea kuita akasikia kitu kama kioo kimeanguka chini na kuvunjika, hakika aligundua kuwa ile ilikua ni flemu ya picha iliyokuwa imetundikwa ndani ya chumba kile, ambayo ni siku moja kabla alimuuliza Msafili kuwa ile picha ni ya nani akajibiwa kuwa ilikuwa picha ya mama mzazi wa Msafili aliyekuwa akiishi hapo kwa mjomba wake na hapo ndipo alipokumbuka maswali yote aliyomuuliza Msafili juu ya kifo cha mama yake ambapo msafili alimwambia kuwa mama yake alikuwa akiishi na kaka yake ambaye ni huyo mjomba wa Msafili lakini siku ya kifo cha mama yake alikutwa amefariki na mwili wake ukiwa umetupwa mtoni, pia baadhi ya viungo vya mwili wake vikiwa vimekatwa, aliyawaza hayo yote ndani ya sekunde tano tu ghafla akamulikwa na mwanga mkali wa taakubwa na ukazimwa ghafla! hapo aliona giza kama limeongezeka mara kumi ya lile la mwanzo, akasikia sauti ya mtu akisema, mfunike usoni haraka....,
Aizaki alijikuta amekamatwa ktk giza ilo na kisha akafungwa na nguo usoni kisha akabebwa na alipojaribu kupiga kelele alizibwa mdomo na kuingizwa kitambaa kigumu mdomoni. wakati huo alisikia sauti ya mjomba akiongea na msafili ..... ukiulizwa sema hujui kitu chochote, wewe sema uliamuka ukakuta hayupo ndani.... Akasikia sauti ya Msafili akijibu sawa mjomba. baada ya hapo akasikia sauti inasema ukiendelea kulia tunakuua, watu hao walimbeba na kutembea kulelekea mahalia asikoelewa lakin baada ya kutembea kwa mda mrefu kama saa moja na alianza kuhisi kuwa walikuwa wakitelemka katika bonde ambalo alihisi kuwa litakuwa ni bonde la mto hapo ndipo alipotambua kwamba kile kifo kilichomkuta mama yake na msafili kilikuwa karibu yake, alijaribu kufikiri njia ya kujiokoa toka mikononi mwa kifo hicho lakini ilikuwa ni vigumu kwake kwakua wakati huo alikua ameshafungwa kamba ktk mikono na miguu yake Aizaki alilia sana lkni hata hivyo sauti yake iliishia ktk kinywa chake ambacho kilikuwa kimezibwa na vitambaa,

Wakati wakiendelea kushuka katika bonde hilo.. Ghafla ulisikika mlio wenye ngurumo kubwa mno ambaoyeye mwenyewe hakuwahi kuusikia ktk maisha yake na wala hakujua ni mlio wa nini, baada ya hapo yule mtu aliyembeba alimtupa chini na akasikia watu walioongoza naye wote wakikimbia huku wanapiga kelele wakisema Simbaaa simbaaaa , kabla hawajafika mbali akasikia wamesimama na kuanza kubishana, sauti ya mjomba wake na msafili ilisema kwa nguvu hapanaaa hamuwezi kumwacha mzima, muuweni kabisa, hapo ndipo Aizack alipotambua kumwa kumbe ile ilikuwa ndio siku yake ya mwisho, likamjia wazo haraka akajifungua kitambaa usoni kwa mikono iliyofungwa na kuanza kukimbia kuingia ktk msitu pasipokujua ni upande gani huyo samba alikuwapo hapo ndipo alipoponea, ule mlio uliendelea kupiga kelele kwa muda kisha ukatulia kwa Aizaki aliona ule mlio kama ukombozi na sio kifo tena hasa baada ya kutambua kuwa kifo kilikua usoni pake.

Alikaa msituni usiku huo mpaka mapambazuko na akaamua kuondoka kuelekea kijijini,
Alipofika kijijini akakuta kuna taarifa zimezagaa mtaani kuwa nyumba ya mjomba wake ilivamiwa na watu wasiojulikana na walimteka yeye Aizaki na kwenda naye kusikojulikana. Hali hiyo ilimfanya aogope kueleza na kusimulia ukweli, na kuhofia kuwa huenda kufanya ivo kungemwingiza katika matatizo makubwa, hivyo hata watu walipomuuliza alijibu ndiyo walimteka wakaenda kumuacha mtoni bila kumdhuru.

Siku iliyofuata alienda shuleni, wanafunzi wote walikuwa wakimzungumzia yeye, alipokutana na Msafili alimwogopa sana kiasi ambacho mwili wake ulikua unatetema, aliamua kukaa kimya bila kumuuliza jambo lolote, Msafili bila aibu alijipendekeza na kujifanya hajui chochote nakumpa pole, lakini kwa Aizaki alizidi kumwogopa na kujitenga naye kabisa.


Akiwa ktk Mawazo hayo mazito Alishituka Akiitwa Aizaki Aizaki ... Upo sawa, hapo ndipo alikumbuka kuwa alikuwa hospitali,
Yule daktari alikua amekuja kumtembelea tena na hatua hii alimwomba kwenda naye nyumbani kwake kwakua alikua yupo vizuri kiafya, Aizaki aliinuka na kuongozana na Daktari lakini kabla hawajatoka mlangoni alikuja Nesi na kumkumbusha daktari kuwa garama za matibabu zilikuwa hazijalipwa, Daktari aliomba waandae bili ya malipo kisha wampe atalipa yeye.
mara baada ya kufika nyumbani kwakwe alimkaribisha ndani Aizaki alikua bado haelewi kabisa alikuwa anaona kama amekuwa muigizaji flani asiyejuwa anaigiza sanaa ya aina gani isiyokuwa na mashabiki. aliandaliwa maji ya kuoga akapewa nguo abadilishe ambazo zilionekana kuwa ni kubwa kwake bila shaka zilikua nguo za yule docta. mpaka wakati huo alikua hajajua kuwa amesaidiwa na nani mpaka kuja pale hospitali, baada ya kukaa Daktari alikuja na kukaa wakaanza mazungumzo,

Aizaki alinza kwa kushukuru kisha akasema kwa sasa mimi sijambo kabisa na angeomba ruhusa aende zake maana hajui kama vifaa vyake vya shambani vilikuwa salama au kuibiwa. Docta akamtuliza akamwambia usihofu kijana vifaa vyako vipo salama kabisa, akamueleza kuwa yeye alikua akipita njiani akaona watu wamekusanyika na aliposimama na gari lake ili kujua kuna nini… ndipo alipoambiwa kuna mtu amezirahi, akasaidiana na watu kumpakia katika gari lake na kumfikisha hospitali. Baada ya mahojiano mengi Docta alipata kumfahamu vema Aizaki na Elimu yake pamoja na mikasa yote aliyo pitia, Kwa Aizaki ilikuwa kama mtu aliyetoneshwa kidonda kwakua alikua akisimulia huku machozi yanatililika kama mtoto.
wakati wakiendelea nan Mazungumzo ghafla Uligongwa Mlango na Mara Docta alipofungua Mlango na wakatokea Polisi.

Habari za Leo tunashida na kijana Aitwaye Aizaki, ambaye alilazwa Hospitali kwa kugongwa na nyoka.

Je nini hatima ya Maisha ya Aizack…..
Usikose sehemu ya Pili

Kwa ushauri na Maoni
Piga Simu 0782982206
Barua pepe danielmtambo@gmail.com


*****************
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom