ni kweli bongo bado sana, lakini ukiwa huko ulaya au america ni vigumu kutoka kuliko ukiwa hapa. hapa kwetu kuna opportunity nyingi sana hasa za kibiashara kwasababu unalipa kodi kidogo na unaweza usilipe kabisa, unaweza kuwa unawalipa wafanyakazi hela ya chini na ukatengeneza faida kubwa, kuna maviwanja kibao yapo yanauzwa bei chee......i will share with you something, ....kitu cha kwanza nilichofanya niliporudi hapa, kwanza kabisa kile kijihela nilichokuwa nasave nilipokuwa kule, nilinunua eneo kubwa zuri kule KAHAMA, nikajenga lodge kubwa nzuri, vyumba kama 20, na kwa bei chee tu, elfu 20 kwa chumba....bahati nzuri, karibia kila siku vyumba vilikuwa vinajaa, within a year, nikawa mtu wa mamia ya mamilioni, wakati nilianza na hela ndogo tu kama dola $50,000.00. unaweza kuanza hata na dolla chache tu kujenga....nilipukutisha kabisa nikaanza kusimamia mimi mwenyewe kama msimamizi/menager wa lodge hiyo....lodge iko mkoani.....piga hesabu kwa hela hiyo elfu 20 kwa siku (ondoa kuuza chakula na nyama choma pale). ...kwa mwaka napata shilingi ngapi? ondoa ile ya labda siku moja moja havijai compensate na faida ninayopata kwa nyama/mbuzi choma na chakula uanzia breakfast hadi dinner pale....ni zaidi ya millioni kama 150 kwa mwaka...ondoa garama mbalimbali za kulipa mfanyakazi na mlinzi etc...kwa namna hiyo kila mwaka nanunua kiwanja na kuongeza lodge nyingine mkoani naweka ndugu yangu pale au mtu ninayemwamini anasimamia kila wili a naniwekea hela kwenye account....sasa nina miaka kadhaa, na nyumba ya kuishi nzuri nilishajenga, na za kupangisha zipo hapa dar....kwa mambo haya ningeendelea kukaa ulaya/america ningejenga wapi? si ningeendelea kufagia, kuosha vyombo na vyoo vya watu, kulea wazee kwenye nursing homes etc...ulaya labda uwe daktari ndo utapata maisha, ila hawa wabeba box wengine,...karaha ya ajabu na huheshimiki kama hapa....unaishia kuangalia na kushangaa utajiri wa wazungu tu...