Kwahiyo kutokea Austria au Australia (thanks for correction by the way) does it make any difference kwamba ni matakwa ya Mungu au sio?,
Sana tu Mungu akinijalia siku nikija Dom naona zitanikoma..., hivi bado zipo kwa wingi?
please naomba unijibu with any good argument kwamba Mungu alitaka hayo yatokee kwa mantiki gani ?
Inategemea ni kwanini sijafika Dodoma ?Je sikutaka kukata tiketi ili nisafiri bure lakini konda akanishika akanishusha?Kwa mfano, refer kwa post yako inayofuata, tuseme umeanza safari ya kwenda Dodoma, na ikatokea hujafika, sababu kubwa itakuwa Mungu hajajaalia ufike Dodoma, huwezi kuconclude eti ni makosa yako kutokufika Dodoma wakati nia yako ilikuwa hiyo.
Kwahiyo watu wanavyotukanana humu JF huwa ni mpango wa Mungu?Una maana gani unaposema nikujibu with good argument? Kama unaona argument zangu sio 'good' ina maana good argument unazijua na unataka kuzisikia kutoka kwangu. Mungu hajapanga bado nikujibu kwa good argument.
Inategemea ni kwanini sijafika Dodoma ?Je sikutaka kukata tiketi ili nisafiri bure lakini konda akanishika akanishusha?
Je nilichelewa kwenda kituoni sababu ya kuchelewa kuamka sababu ya kutokuseti alarm?
Je badala ya kukata tiketi mapema nimengoja mpaka last minute nikakuta tiketi zimekwisha?
Je badala ya kupanda basi ili kusave pesa nimeamua kwenda na baiskeli nikashindwa kufika sababu nimechoka
Badala ya kupanda basi la kwenda Dom kwa makosa yangu nimepanda basi la kwenda Arusha...
Mkuu on all the above issue naona kuna jambo moja tu ambalo limesababisha mimi kutokwenda Dom na kushindwa kula zabibu? nao ni uzembe wangu mwenyewe..
Kwahiyo watu wanavyotukanana humu JF huwa ni mpango wa Mungu?
Sijasema Mungu hausiki katika maamuzi..., namoumba Mungu niamke siku hiyo na Nguvu na bila matatizo.., ila kuzembea kwangu kuseti alarm ili niamke na kupanda basi la Arusha badala ya Dom siwezi nikalaumu kwamba Mungu hakutaka niende DomBasi usimshirikishe Mungu kwa kusema Mungu akijaalia. Sema nisipofanya uzembe nitakuja Dodoma kula zabibu.
Kwahiyo kipimo cha mke/mume kutoka kwa Mungu au kutokutoka kwa Mungu ni furaha au huzuni katika ndoa ?, Kumbuka kuna mambo ambayo hayavumiliki mfano abuse (mental and physical) sidhani kama Mungu atapenda yeyote akumbane na haya majanga, na hawa wanaopiga wake zao nadhani ni ushetani/ukichaa uliowakumba ukubwani
Je hawa tuseme Mungu amewatenga ili wasipate wenza wao, au atawachagulia watakaovumilia kuwa abused ? Na ninajua kuna Dini haziruhusu Divorce.., je unapogundua kwamba huyu sio chaguo la Mungu utafanyaje ili uombe Mungu akupe chaguo lako?
Kipimo cha furaha na Amani katika nyumba ni UWEPO WA MUNGU KATIKATI YENU. Ni namna gani mnamshirikisha Mungu katika furaha na shida zenu.
NI vipi mnamuona Mungu wa maana katika kusimamia maisha yenu.
Hata kama unafika mahali unashindwa kuishi na mwenzako, lakini ukiwa uko karibu na Mungu atakuongoza ufanye nini, uondoke,
au amrekebishe amuumbe upya ili mfanane?
Kwa hiyo mimi bado naamini Mke/Mume Mwema kwako/kwangu lazima atoke mikononi mwa Mungu, ili awe sababu ya furaha na Amani yangu.
Hapo kwenye Bold unasema Mambo yakienda Vibaya kwenye Ndoa tunaweza kuomba Mungu ambadilishe mwenza, au uondoke (divorce)...., Je huoni hiyo ni kama short cut ya sisi kutokuvumilia shida zetu na kuachana kwa kusema kuwa Huyu hakuwa chaguo la Mungu... Ofcourse majaribu yapo na ndio maana wana Israel waliendelea na safari yao wangesema haa tumechoka ngoja turudi..., Je nao wangeweza kusema kwamba Mungu Hakutaka tufike ?
Point yangu ni kwamba binadamu wengi wameshajiwekea excuse kwamba mambo yakiharibika wanasema ni upendo wa Mungu wakati kumbe hawakufanya bidii mpaka mwisho wa kipimo chao.., je unakumbuka ile hadithi ya talanta (vipaji) ambavyo walipewa watu ili wazalishe.., mwingine akaziweka, mwingine akazalisha na mwingine akazitumia na kupata hasara ?
Na haya mambo yamekaa kiimani zaidi, inatakiwa kumwamini Mungu na utendaji kazi wake, kuelewa ukuu na uweza wa Mungu pamoja na kuamini kuwa yeye yupo na anafanya mambo. Binafsi naamini hivo.
Ni kweli haya mambo ni ya imani zaidi, na Mungu anaweza yote.., umesema labda ukipata Mme ambaye sio chaguo la Mungu anaweza akakutoa kwa Gharama yoyote (lakini huoni kwamba mambo yote yanayotokea kwenye ndoa ni majaribu ambayo yapo kwenye ndoa zote na inabidi tuyategemee na tushukuru tu kile tunachopata) Mfano ukifiwa na Mwenza... (Binadamu wote tutakufa.., hilo ni jambo la kawaida na sio kwamba litakukuta peke yako ila ni kuomba litokee later na sio sooner)."[/SIZE]
Nampenda Mungu Pia LD;Na kuna mwingine hawezi kutokana na jinsi alivyoumbwa na kiwango cha Imani yake, basi Mungu anamfungulia mlango anaolewa tena.
Daaa matendo ya Mungu yanatisha kama nini. Na Mungu hafanyi mambo kwa kubahatisha, hasa ikiwa umekabidhi maisha yako kwake na unamwamini asilimia mia moja. Nampenda Mungu.
Nampenda Mungu Pia LD;
Hivi huwa tunaumbwa na Imani au tunapata Imani ulimwenguni kutokana na Mafunzo ? (mfano ningezaliwa China huenda ningekuwa Budha, India ningekuwa Hindu na Imani zangu zingekuwa tofauti)
Na kwa mtaji huo kama tuna excuse ya kutokea kwamba makosa haya ya ndoa kuharibika ni sababu ya kuwa na mtu ambae Mungu hakunipangia..., nitatofautisha vipi kwamba sio shetani ameingia kwenye ndoa au ni majaribu ambayo Mungu ananipa au sisi wenyewe kukosa maadili ya ndoa au ujana unatusumbua ?