Who made space,universe and our world

Vitu vyote vinetokea by chance otherwise uwe na uwezo wa kunitajia huyo aliyemuumba mungu anayetajwa. Biblia ni kitabu kama vitabu vingine
 
The answer is ..who do you think? There are many theories which are advocating the origin of the univese more specifically GOD as the creater ..the question is who created him(GOD)
 
The answer is ..who do you think? There are many theories which are advocating the origin of the univese more specifically GOD as the creater ..the question is who created him(GOD)

Vitu vyote vinetokea by chance otherwise uwe na uwezo wa kunitajia huyo aliyemuumba mungu anayetajwa. Biblia ni kitabu kama vitabu vingine
Mkuu kitendo cha kilichoumbwa kutafakari au kuuliza juu ya uhalisia wa Muumba ni kitu ambacho kwenye calculator hutokea kama "Math Error" ambayo kwa lugha ya ki-calculator ina maana ya beyond the capabilities yaani juu ya uwezo wa kifaa husika.
Huyu Mungu Muumba wetu kwa maneno yake mwenyewe akiongea na mwanadamu (Musa) Alimueleza juu ya asili yake kwa lugha ambayo tafakari ama fikra za binadamu zingeweza kudadafua Alijibu kiufupi tu kuwa " I AM WHO I AM " yaani Mimi Ndiye ambaye Ndiye kumbuka kuwa upeo wetu wa kufikiri una mwisho hivyo sisi kuelewa asili kamili ya Muumba kuwa yeye Ndiye Aliyekuwako Yupo na Atazidi kuwepo ni ngumu sana kuinyaka hasa ukiweka dhana kichwani kuwa sisi ni wadhambi na hivyo mambo ya Utukufu wa Mungu kwetu ni ngumu kuelewa lakini bado Mungu hakutaka sisi tubaki gizani na hivyo Alisema kiurahisi kwa lugha rahisi ili sisi (Kifaa hafifu) tuelewe.
 
Umeeleweka kwa waelewa.

Kwanza lazima ujue kuwa sisi wanadamu tuko Limited katika mambo mengi mno.
Mfano, kwanini tunashindwa kusafiri hadi kulifikia Jua.

Ni kwamba tutaungua kwani mwili wetu ni dhifu kuliko Jua ambalo liko imara na lina nguvu nyingi.

Huo ni mfano mdogo tu.

Sasa kwa upande wa kuelewa mambo sisi wanadamu tuna milango mitano inayopimika ya kuelewa mambo.
Yani kupitia Kusikia, Kuona, Kugusa, Kunusa na Kuonja, wengine wanasema wanauwezo wa kupata taarifa kupitia Kuhisi na Kutahajudi (kumeditate)

Sasa kama ni hivyo inaamaana njia za ufahamu ziko hizo tu ?
Vipi hiyo milango mingine ya ufahamu ambayo hatuijui tutapataje maarifa yake kupitia kwayo ?

Mi najua kuna mamilioni ya milango ya ufahamu lakini sisi wanadamu hatuwezi kuifikia kutokana na maumbo yetu yalivyo.
Kuna baadhi yetu ni walemavu wa masikiao na macho hivyo wamebakiza milango mitatu tu ya kufahamu mambo.
Hao hawaujui upinde wa mvua ulivyo maana haugusiki wala kunusika wala kuonjeka.

Mungu yupo na ameshasema kuwa kutokana na umbo la mwanadamu lilivyo dhaifu kiasi cha kushindwa hata kulisogelea Jua, hatuwezi kumwona na akijitokeza kwetu tutakufa.
Pia hatuwezi kumwelewa zaidi ya alivyotueleza mwenyewe kwakuwa tunahitaji milango mingine ya ufahamu ambayo hatuna.
Wewe una vimilango vitano tu vya ufahamu na unataka uelewe kila kitu.
Jiongezee basi milango mingine ya ufahamu ili uelewe mambo mengine, vimilango vyenyewe umezawadiwa tu, kikifa kimoja huwezi kukirudisha ni kama umefadhiriwa tu halafu unatunisha mgongo.

Mungu yupo Someni Biblia mtaelewa anavyosema.

Full Stop.
 

We umedata tu na dini mkuu, sayansi haihitaji muongozo wowote wa dini maana dini ni full uongo, sayansi ikifata muongozo wa dini itafeli. Vitu vingi vilivyoandikwa kwenye vitabu vya dini hasa bible na quran ni vitu impossible, paradoxes kibao, yaani hata mjinga akisoma anajua anadanganywa.
 
Hapa mm napita tu niwahi kupima afya ma meri yetu inatusibiria
 
Mfano mdogo tu mkuu kwenye Biblia Mungu Aliwaambia wana wa Israel kuwa washikapo mzoga yaani mwili wa mwanadamu au mnyama aliyekufa waoshe mikono yao kwenye maji yanayotiririka "Running water" hii wapasuaji wa kwanza (wanasayansi) walikuja kujua baadae na ni baada ya watu wengi kufa kisa daktari mpasuaji ailikuwa akifanya upasuaji na kisha kunawa kwenye maji yaliyoko kwenye beseni yaani still water kwa hiyo alirudi kufanya upasuaji mwingine na bakteria lukuki mkononi na huku kwenye Biblia Mungu aliwaasa wana wa Israel karne nyingi sana kabla.
Wewe huoni tatizo hapo mkuu ndio maana wazee wa kale waliona umuhimu wa elimu ya Neno yaani theologia kwa sababu ilikuwa ngumu kwao kufanya uvumbuzi stahiki na wenye usalama kwa maisha ya mwanadamu bila kwanza kujua Neno linasemaje.
 
Sasa wewe tuambie ulimwengu ulikotokea hadi hapa ulipo sasa hivi,Iyo sayansi yako inasemaje?.Yaani kutaja mapunguvu ya kiimani hakukufanyi wewe na syansi yako uwe sahihi,Kinachotakiwa ni wewe kuleta hoja fikirishi za kisayansi ili tukuone una hoja,Ukikomalia kejeli tu haitoshi,Otherwise na sisi tutakuona tapeli tu.
 
Tukitumia sayansi pekee kuuliza kuuhusu uumbaji huishia unknown forces au suppernatural power
 
Daahh umetoka lini MILEMBE
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…