salisalum
JF-Expert Member
- Oct 27, 2010
- 434
- 159
Ndugu Watanzania naomba tutafakari hii hoja iliyoko kwenye swali, nani hasa kwa sasa anaongoza nchi yetu?
Kwa nini nimeleta hii hoja? Nina sababu kadhaa ambazo nitazitanabaisha hapa chini:
1. Ndugu Samia Suluhu Hassan akiwa bungeni mara baada ya kujitangaza mshindi katika uchaguzi ambao kiukweli haukufanyika, aliwaomba wajumbe kwenye ukumbi wa bunge wasimame na kukaa kimya kwa muda kuwatambua na kuwakumbuka watu wote waliouawa kuanzia tarehe 29/11/2025. Samia huyu huyu akiwahutubia watu wanaodhaniwa kuwa wazee wa Dar es salaam hakuwataka hao wazee kusimama na kuwakumbuka hawa marehemu. Katika hotuba yake alionyesha kuchukizwa sana na victims hawa huku akiwatuhumu kutaka kuiangusha serikali. Alisema pia nguvu iliyotumika (kuua) ilikuwa sawa. Haiwezekani kiongozi akawa na hizi extremes mbili kwa wakati mmoja. Haiwezekani kuwa na kiongozi anayetaka kuwangoza watu kuvuka dhahama na sintofahamu iliyotokea lakini wakati huo akiwa kachomoa upanga.
2. Waziri wa mambo ya ndani amesikika hivi karibuni akiwaagiza polisi waache kukamata watu bila kufuata sheria. Waache kukamata watu wakiwa bila sare zao rasmi, waache kukamata watu wanaotuhumiwa kwa makosa madogo kama makosa ya mitandaoni usiku wa manane huku wakiwa na silaha nzito, na mengine mengi. Hata hivyo ukamataji usiozingatia sheria bado unaendelea kama ilivyokuwa na ukamataji kwa namna ya utekaji unaendelea. Haiwezekani kama nchi ina uongozi ukafanyika upuuzi wa namna hii.
Kama polisi hawamsikilizi waziri wa sekta yao wanamsikikiza nani?
Who is really in control?