Koba said:...mkuu taratibu hapo,nafikiri ni vizuri kuweka emotions pembeni na kuangalia facts za pande zote la sivyo vita itaendelea,na inaonekana kwako verdict ni tayari na Nkunda is a war criminal na Rwanda ndio Nkunda,na unaamini Nkunda sio Congolese ila ni tutsi wanaotaka hima empire in great lakes,na inaonekana huelewi vizuri hii saga ndio maana umebaki kushutumu upande mmoja tuu,hakuna mtu mwenye interest ya vita au kuchukua nchi ya mtu mwingine,security ndio issue kubwa hapo...sijui kama unaweza kulala kama adui yako ambaye ameua watu almost a million kasimama next door walking freely,sijui kama wewe ungekuwa Kagame unge deal vipi na Hutu extemist ambao sasa wamepiga camp Congo wakisubiri muda muafaka kuvamia Kigali na Kabila hawafanyi chochote,na wakiamini mtutsi yeyote duniani ni adui yao,tatizo sasa limekuwa more complicated in Congo(politically) maana propaganda ni kwamba banyamurenge(almost a milion) sio congolese,sasa sijui unataka Nkunda Banyamurenge waende wapi au walale wasubiri waje kuchinjwa(that will never happen my friend)..kabila kama ni kiongozi wa wacongo wote lazima ajue kina Nkunda wana legitimate issue wanayopigania na lazima awahakikishie usalama wao na aache propaganda za kuwafanya Banyamurenge kama sio raia halali wa Congo la sivyo security wataitafuta wenyewe na sitashangaa kabila akaishia kuwa mkimbizi na yeye!
Nkunda ni mzaliwa wa kongo!hii serikali ya Congo si iwatambue tu hawa banyamulenge yaaishe!Nasikia hii issue ya kutowatambua ilikuwepo hata enzi za Mobutu!
Na hawa ndo walimsaidia kabila kuingia madarakani alipoingia na yeye akawageuka tena!Sasa na kabila mtoto anaendeleza yale yale!
Inakuwa vigumu kwa mgeni kumlazimiasha mwenyeji wako akuruhusu uwe mwenyeji. Ingawa ina historia ndefu, Issue ya Banyamulenge iliibuliwa na Kagame, lengo lake ilikuwa ni kumuondoa Mobutu, na hatimaye kumfanya mtusi awe kiongozi wa Kongo, lakini hesabu zake ziliharibika na wakongoman wakawastukia. Kabila hakuwageuka watusi(banyamulenge) ila hakujua nia yao halisi, yeye mwanzoni alidhani kuwa ni kweli nia yao ni kumuondoa Mobutu aliyetuhumiwa kuwa anawahifadhi wahutu(interahamwe) na alitaka kutumia opportunity hiyo kufanikisha ambition zake za kuwa Rais, kumbe nia yao ya ndani ilikuwa ni kumtumia kumuondoa Mobutu na kumuweka madarakani kwa muda, na baadaye kumuua na nafasi achukue Bizimana Karahana mtusi ambaye angekuwa Rais wa Congo. Bahati mbaya au bahati nzuri wakongoman wenye akili wakaamua Kabila mdogo aingie madarakani badala ya Karahana, ili nchi isiuzwe.
Wanaosema kuwa Kabila sio Mkongoman kwa sababu haongei kifaransa huo ni ujinga, kifaransa sio Kikongo ni lugha ya nchi moja huko Ulaya ambayo inaongewa na watu wa nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Kongo. Utata wa uraia wa Kabila uko kwenye upande wa Mama yake ambaye inasemekana ni mtusi, lakini wanaoleta hoja hiyo ni wale watu mufilis kisiasa na wenye uchhu wa madaraka kwa kisingizio cha uraia wakati hawana uwezo.
Kabila amekulia nje ya Kongo kwa hiyo ni kawaida kwa yeye kutojua kifaransa, na ni kweli amesoma Tanzania na ameishi Tanzania na ndugu zake wameishi na kukulia Tanzania, but that does not make him not a congolese. Kwa hiyo anachosema Shy hakibebi maji.
Very interesting observation.
Bongolander,
shukran sana kwa kutuelimisha on the chain of events of this quagmire.
Swali linakuja hivi, mbona Joseph Kabila asiwaamuru hao Interahamwe(Hutu)
warudi Rwanda and let the UN monitor their protection over there under a
different auspices? Iwapo hawa jamaa watabaki DRC basi Kagame will have
a legitimate reason of trying to get them even if its by proxy.Na hapo ndo
hii kasheshe haitomalizika.He believes the guys will regroup na warudi Rwanda
kumngatua mamlakani.
It is very obvious Kagame backs General Nkunda maana hata baada ya vipress
conference vyake na ule mkutano na Obasanjo,jamaa anaelekea Kigali in full
glare.Kisha over there, no efforts are made to reprimand him even though ni
mshukiwa wa War Crimes kibao.
Unajua Congo ina msingi wa kisheria wa kuwafukuza watusi(banyamulenge) kwa kuwa sheria yao ya uraia inafuata mkondo wa damu(jus sanguinis) na haifuati sehemu ulipozaliwa. Kwa hiyo kwa mujibu wa sheria za Congo watu kama Nkunda ni wageni. Lakini Kabila na wakongo hawana uwezo wa kuwaamuru waondoke kwa sababu hawana means za kutekeleza amri hiyo.
Kitu kingine muhimu unachotakiwa kuangalia ni kuwa Juvenal Hyabyarimana aliwafukuza watusi wakakimbilia Congo, Uganda na Tanzania na wengine kidogo Burundi, baada ya Kagame na Kanyarengwe kuwaorganise watusi kutoka sehemu hizo wakatungua ndege ya Hyabyarimana na kuivamia Rwanda, nao wakafanya mauaji ya halaiki kama ingawa si kwa kiasi kikubwa kama interahamwe, na kwa ujumla walipanga kuwafukuza au kulipiza kisasi kwa wahutu. Kwa hiyo sasa kumekuwa na makundi mawili ya wanyarwanda nchini Congo (wahutu-interahamwe na watusi-Banyamulenge). Kagame anahofu kuwa kuna siku nao wahutu watakuja kuwa organised (which will happen) warudi tena Kigali kama alivyofanya Kagame. Nkunda anatumiwa kuwadisturb na kuwamaliza mmoja baada ya mwingine, hii ndio mission iliyobaki sasa baada ya kushindwa kuweka rais mtusi Congo. UN nayo haina nguvu ya kutosha kuweka ulinzi, maana jimbo la Kivu Kaskazini ni kubwa sana kijiografia na halina infrustructure ya kuruhusu easy movement ya vikosi. Kwa hiyo ndio maana guerillas wanaojua njia za panya wanatesa zaidi.
Ukifuatilia vizuri historia ya Zaire utaona kuwa Mobutu alikuwa anavuna tu wala alikuwa haongozi, hakujenga barabara na miundo mbuni mingine, ndio maana nchi ndogo kama Rwanda inaweza kumchezea Kabila kama inavyopenda, sababu ni kuwa serikali ya Kinshasa haina nguvu na infrustructure ya kutosha kutawala na kudhibiti nchi, hiyo weakness watusi wanaifahamu vizuri sana
.....mawazo kama yako ndio yanafanya watu kama mimi niwaunge mkono kina Nkunda na wenzake,hii idea ya kuwafanya kina nkunda sio Congolese ni hatari sana na ndio sababu kubwa ya vita,sijui hata kama unajua history ya banyamurenge? hii bullshi-t ya kutaka kuwa drive out almost a million banyamurenge out of Congo kwa kutumia jus sanguinis non sense nafikiri ni uwendawazimu wa hali ya juu,na sijui waende wapi? part kubwa ya yeye kabila leo kuwa Raisi ni hao banyamurenge maana ndio waliopigana na mobutu which led to bringing his father to power,leo kawa raisi eti nyie sio raia (WTF?),na alivyokuwa mpuuzi kaanza kuwatumia interahamwe kuwaua banyamurenge (raia wake mwenyewe),Nkunda principally is fighting for his security and freedom la sivyo watafanywa stateless citizen na kuchinjwa wote....interahamwe wapo makini wanasubiri their chances kuwasafisha banyamurenge!
jamani chanzo cha ugomvi wa wahutu na watusi ni nini?
Koba unajua ukweli ni kuwa kila nchi inasheria yake. Sheria ya uraia wa Congo haitokani na mtu kuzaliwa kwenye ardhi ya Congo, bali inatokana na damu yake. Kama Ukizaliwa Congo na huna damu ya Kikongo basi wewe si Mkongo, kama ukizaliwa nje ya Congo na una damu ya Kikongo basi wewe ni Mkongo, ndio maana nasema kisheria Congo ina haki ya kimsingi kuwafukuza Banyamulenge. Nadhani hata Tanzania tunafuata sheria hiyo, lakini pia mtu anaweza kuomba uraia, sasa kunyimwa au kupewa ni uamuzi wa mwenyeji. Kama jus Sangunis wewe unaona ni non sense well and good lakiniinatakiwa kuheshimiwa hadi itakapoondolewa.
Wale jamaa sio stateless, ni wanyarwanda na ndio maana Kagame haawachi. Lakini cha ajabu wanyarwanda wengine yaani wahutu interahamwe anataka wachinjwe. Na for sure kweli jamaa watajiorgnaise watarudi tena, and the cycle will go on and on and on.
.......Banyamurenge tutsi have lived in Congo for well over a century,walikuwepo pale kabla hata ya Berlin conference,just kwa sababu kuna watu the other side of the border wanao share language & culture basi wao sio congolese,kabla ya kuja hapa na kuongea vitu usivyokuwa na uhakika navyo ni bora ukasoma history kidogo haiumizi!
sawa mkuu nina hakika kabisa kuwa kuna wakongo watusi, na kuna watanzania watusi ambao baadhi yao waapear in form ya hawa na wahaya na wengine wengi tu alike. Hao si wageni, ninaowazungumzia ni wale waliokimbizwa Rwanda baada ya genocide ya kwanza. By the way mimi ni mvukutu najua historia ya hii kitu kutokana na first experience. Thanks for advice anyway.