Who is Fahmi Dovutwa?

CCM inalea mafisadi - Dovutwa



na Deogratius Temba




VITA dhidi ya ufisadi nchini haitakwisha kwa kuwataja tu kwa majina watu wanaotuhumiwa bila kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria vinavyohusika.

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha United People's Democtatic (UPDP), Hahim Dovutwa, alipokuwa akitoa msimamo wa chama chake kuhusu suala la ufisadi lililokithiri nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Magomeni Mwembechai, Dar es Salaam, mwenyekiti huyo alisema kuwa, umefika wakati kwa kila Mtanzania kuamka na kukemea suala hilo, bila kuogopa na kutishika na kauli zinazotolewa kuwa mijadala imefungwa.

Dovutwa alisema UPDP inakubaliana na harakati za kupinga ufisadi zinazoendeshwa na baadhi ya wabunge wa upinzani, kwani kwa kiasi kikubwa zimeleta ufanisi na mabadiliko makubwa ya kisiasa na kiuchumi.

Alisema kinachotokea sasa ni majina hayo kutajwa na kuwa siri, badala ya kuyapeleka katika vyombo vinavyohusika, ikiwa ni pamoja na Wana-CCM wanaotajwa kuhusika na ubadhirifu kushindwa kuwajibishwa ndani ya chama chao.

"Nilitaka CCM ituambie kama kweli inachukia ufisadi, imepeleka watu wangapi mahakamani, na wanachama wake ambao wanatuhumiwa na ufisadi, wamefukuzwa au bado wanaendelea kukumbatiwa? Watuambie tumemfukuza fulani kwa sababu za ufisadi, sisi tutajua kweli wanauchukia," alisema.

Aliwataka wabunge wa CCM kutotumia ajenda ya ufisadi mahali popote kwa lengo la kujijenga kisiasa, kwani wao si waanzilishi wa hoja hiyo na hawawezi kupigana na ufisadi wakiwa bado ndani ya CCM.

Aliongeza kuwa hoja hiyo iliasisiwa na Mbunge wa Karatu, na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilibrod Silaa, na si wabunge wa CCM ambao wameidandia.

Aliwataka wabunge wanaosema kuwa CCM yao imekumbatia mafisadi waondoke, kwani siasa ni popote.
 
Wabunge CCM hawana ujasiri, asema Dovutwa
Na Khamis Mkotya

MWENYEKITI wa Chama cha United Peoples' Democratic (UPDP), Fahmi Dovutwa, amekiponda kikundi cha wabunge wachache wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliopo mstari wa mbele katika vita dhidi ya rushwa na ufisadi, akisema kuwa wabunge hao hawana ujasiri wa vita hiyo zaidi ya unafiki.

Dovutwa ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu, ameibuka na kuzungumzia masuala mbalimbali, huku akiwashauri wabunge hao wa CCM kukihama chama chao iwapo wanachukizwa na vitendo vya rushwa na ufisadi ndani ya chama chao.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisini kwake Mtaa wa Kagera, Mwembechai, jijini Dar es Salaam, Dovutwa alisema kuwa wabunge hao wanapoteza muda kwa kuendelea kupigia kelele suala la rushwa na ufisadi wakiwa ndani ya CCM.

Dovutwa alisema, CCM haina dhamira ya kweli ya kupambana na vitendo hivyo kwa kuwa tangu kelele hizo zianze kupigwa chama hicho hakijachukua hatua zozote dhidi ya wanachama wake wanaotuhumiwa na kuthibitika kuwa ni mafisadi au wala rushwa "Wanatwanga maji kwenye kinu," alisema.

Dovutwa aliwataka wabunge hao kuiga mfano wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu Profesa Kighoma Ali Malima na Waziri wa Mambo ya Ndani, Augustine Mrema, ambao waliacha nyadhifa zao baada ya kuchukizwa na mambo ndani ya chama hicho.

"Katika miaka ya hivi karibuni, tumewaona watu waadilifu ambao kweli walikuwa wamechukizwa na yaliyomo ndani ya CCM wakaamua kujitoa na kujiunga na vyama vingine.

"Hawa ni pamoja na marehemu Profesa Kighoma Ali Malima, Augustine Lyatonga Mrema tena wawili hawa wamejitoa ndani ya CCM wakiacha nyuma nyadhifa za uwaziri kila mmoja. Hawa kina Kilango wao ni wabunge tu," alisema.
 
These type of people are f***g disgrace!..
Goin on tv bitching like that...Sasa kwa nini alitaka kugombea urais kama alijua kikwete anafaa?
kwa nini kaanzisha chama cha upinzani kama ccm is cool?
kwa nini hakufunga mdomo wake basi kama walimkosea jina na kumkosesha hela?
GRRRRHHHH....AKHH njaa hizi tabu sana,njaa zitatumaliza watanzania

Ndo maana mara ya mwisho alivyoojiwa mama yake huko msanga alidai kuwa hafaham kama mtoto wake anagombea kupitia chama ghani.
These clones sucks big tym!
 
Alilazwa Nkwezi dispensary,magomeni Mapipa alivyokarabia kufa CCM wakampeleka REGENCY hospital,analipa fadhila....
 
Tujuzeni zaidi wakuu lakini tupeni data zenye uhakika na ambazo haziegmei upande wowote na zisiwe na jazba ndani yake.
 
kaishia kidato cha Nne,lkn hata mama yake mzazi alikuwa hajui kama mwanae anagombea uraisi mwaka jana,ni mfanyabiashara wa hardware pale gerezani,kashindwa kumshaWishi hata mama yake mzazi ajiunge Na chama chake.
 
Back
Top Bottom