Who is Benno Malisa?


Mkuu Son of a Peasant, Heshima mbele...
Sitaki kupinga hoja zako, hasa kwa kuzingatia kuwa umesema kuwa ni rafiki yako na unamfahamu kwa karibu sana, pengine kuliko mchangiaji mwingine yeyote. Hata hivyo, kuna hoja ambazo ni controversial kwenye post yako, naomba ufafanuzi...

Kwamba Benno ni mkimya, na ana maadili... nadhani hili ni relative term, kwangu mimi Benno sio mkimya, wala sidhani kama ana maadili kihivyo. Huyu jamaa, nilikuwahi kukaa naye Makuti Hotel, mjini morogoro, kwa kama saa mbili hivi. Alikuwa anasafari ya Dodoma I think, na alipita pale kukutana na rafiki yake ambaye walisoma pamoja huko sekondari, na kwa kuwa huyo rafiki yake ni rafiki yangu pia, nilijikuta nikiwa katika ya mazungumzo yao. By then (2006 au 2007), sikumpa attention sana kwa kuwa hakuwa kiongozi, but nakumbuka sana maongezi yake, stori alizokuwa anapiga, staha na haiba yake... kwa kweli kusema ni mkimya, au ana maadili... kwangu mimi hakukaribia kabisa viwango.

Pili, kuwa Benno hajanunulika... mh, unless unipe strong evidence ndugu yangu, maana hata kwama umeongea naye, usidhani angeweza kukuambia hilo... Lakini ushahidi wa kimazingira, kutokana na kauli ambazo ama anazitoa mwenyewe dhidi ya wapinga mafisadi (ndani na nje ya CCM), kwa kweli itakuwa ngumu sana kusema kuwa ni 'mtazamo' wake, hasa ukizingatia anaoelekea kuwatetea.

Tatu, kusema kuwa Benno ni 'kichwa' napata kigugumizi kidogo. Kama Benno ni kichwa, na kama alilelewa katika mazingira ya utulivu na yasiyo na bughudha za kimaisha, nungetarajia angefaulu darasa la saba pale Himo primary... Kwa nini alifeli??????????? .kufeli hapa namaanisha hakuchaguliwa kuingia sekondari za serikali, kama Old Moshi (ordinary) au akina Ilboru (special) n.k. Kumbuka kipindi kile hakukuwa na shule nyingi za kata, na shule za serikali zilikuwa zinaheshimika sana. Inawezekana kuwa ni kichwa kweli lakini pengine kutokana na umapepe, na kutokutulia kwake (kinyume na ulivyotuambia) akawa hazingatii masomo, akashindwa kupata maksi za kwenda government...

Kweli hana msimamo? Mbona kama anasimamia upande wa mafisadi?

Nasikitika siku ile vilipokuwa vinatoa tamko la kumtukana Slaa, kabisa niliamini Benno hakuhudhuria kikao kile, lakini nilikuja kuishiwa nguvu kuona kuwa alikuwepo, tena ndiye aliyeongoza kikao!!!, ambapo Rz1 hakudhuria...

Son of a peasant... come again my friend.
 

Benno is a good boy
 
Tuulize sisi tukwambie huyo Kiongozi wako Mbowe enzi zake wakati anafukuzia wanadada pale kwenye lango la Jangwani. Mbona sasa Mwenyekitu.

lazima ujuwe watu ubadilika

Umetumwa.....
 
Beno ni kijana makini sana. Ameona hali ya chama chake inakwenda mrama, viongozi wanaotakiwa wachukue hatua hawafanyi hivyo, ndiyo sababu kaamua kuchukua hatua kwa kuanza kuwalipua wenyewe. Hata JK amelipuliwa, hivyohivyo Lowassa, Makamba, Rostam na wengine ambao wanaonekana ni kikwazo cha chama. Sababu kubwa ni kulindana na kutokuchukuliana hatua za kukinusuru chama.

Hivi mnataka naye akae kimya ili chama kife. Huo ndio mwanzo wa kujitoa gamba kwa CCM. Tusubiri tu tuone tusimlaumu, pengine baadaye tutaweza kujua kwa nini anafanya hivi. Kwa kawaida Beno huwa si mzungumzaji sana katika siasa.
 
Mmmmh!!! Tumeshindwa kujiokoa kama watz na sasa mungu ameamua kutusaidia wagombane wao kwa wao na mwisho ccm itakufa na tanzania tutakua huru tena nasi maskini wa siku zote tutaonja mema ya nchi tuliyoyakosa toka 1985(ruksa,bm na sasa jk) mungu ibariki tz na walaani wote wanaoinyonya
 
Tuulize sisi tukwambie huyo Kiongozi wako Mbowe enzi zake wakati anafukuzia wanadada pale kwenye lango la Jangwani. Mbona sasa Mwenyekitu.

lazima ujuwe watu ubadilika

Ndugu yangu Hafif una matatizo sana! mbona hoja zako mara nyingi ni pumba tu. Kwanini unatoka kwenye hoja ya msingi unaanza kuingiza unazi wako? Kama huna hoja kwenye topic iliyopo achana nayo tumia muda wako kwa mambo ya msingi zaidi kaka/dada.
 

Huyu kijana amenunuliwa akanunulika. Amekwisha kisiasa.:lol:
 
Hebu wenye kumfahamu huyu kijana na kinachomfanya ajiamini watujuze... ni pesa said:
Kwa taarifa nyeti, Benno ni kuwadi mkuu na mtaalam wa kuopoa totoz wanaojipitisha kwa JK.
 
au wale mabaa medi pale BOMA LA NG'OMBE

... moral authority kakupa nani braza? Besides kama anafukuzia huko wewe inakuwashia nini pilipili usiyoila? Bahati mbaya sana kwa hili hakuna mtakatifu, kwani wewe kama ni dume hujawahi kufukuzia hiyo habari. Unafiki acha braza. Its below the belt.
 
Nimakamu mwenyekiti wa uvcc......siyo cheo kidgo kwenye sisas za cham tawala.......siasa ni maisha ya binadamu ina kupanda na kushuka..uwezi kua kama malaika...nikijana anayejifunza uongozi siku baada ya siku..kwahyo hyo nisafri yakendefu.......nadhani kutokana na mabadiriko makubwa ya mfumo wetu wa uchumi,akina mallisa imekuachangamoto kwao sana kiasi cha kushindwa kua imara kwa mfumo hupi na filosofi hipi aifuate,,pia viongozi waliomzunguka ni watu waaina gani?kwahyo yanayotokea kwa uvcc na malisa ni result ya umfumo huu unaofuatwa na viongozi wa cham tawala...........kama kanunu na taratibu za cha hazifuatwi inamaana waakina malisa watakua watu wa ainagni?
 

Yaani ni kweli kabisa haujakosea. you are very serious
 
Jaribu kuwa makini na lugha ya watu; gay na guy ni maneno mawili tofauti. Gay ni tusi kubwa ndugu yangu. And what is discusing the issue? Perhaps you meant discussing the issue.

Acha uongo gay sio tusi ni sifa ya mtu, gay=******, hili sio tusi ni sifa au tabia, au hujui tofauti ya tabia mbaya na tusi?? tafakari, chukua hatua.
 
..Mimi ninachojua amepaa hadi alipo kutokana na FADHILA YA RIDHIWANI KWA KUMSAIDIA SAAAAAAANA DARASANI..hilo hata wote waliosoma nao hao wawili degree ya sheria hapo Mlimani wanalijua..I doubt kama ipo siku atakuwa na independent thinking-when it comes to politics alizoingia kwa mgongo wa Ridhiwani....si kwamba ni kilaza, ana akili (though zaidi pia za darasani)....
Poor him!...ni kama jamaa mmoja anaitwa Daudi Deo-aliyekuwa Rais wa DARUSO- 2007-2008, ana akili pia, lakini poor him pia 'hajiamini na anaamini katika kubebwa bebwa..watu kama hawa walikuwa very potential kwa Tanzania ijayo..lakini maskini hawauamini uwezo walio nao, thus wanakuwa mabua ya kutumika!..am just very sorry for them..
 
sasa kama kwenye ukuwadi wake kwa jk alikuwa anawapitia pia hao mabinti baadaya bosi wake atajiju! atawafuata akina Amina chifupa
 
Benoooooo Malisa ndiyo alikuwa chaguo la Ridhiwan katika uenyekiti wa UVCCM, babaye akapiga stop baada ya kuona sasa kisiasa kiti kihamie Zenj. Na walipotapa opportunity tu ya weakness ya Masauni (kugushi umri) kampeni zipiigwa chini chini kwa nguvu zote ili kumtoa Masauni, zote hizi manager akiwa Benno, na Riz vuvuzela. Riz hawezi kufanya uamuzi wowote technical bila kusaidiwa na Benno. Wote Benno na Riz ni set elements za Universal set MAFISADI hasa Lowassa na Rostam. Bashe anachapia pale hasa inapokuja issue ya Rostam ambaye ndiye mfadhili na mwajiri wake kule Habari Corporation ambako kumedoda pia. Hivyo jamani Benno wa jana si wa leo, ameshanunuliwa na wenye nchi. Ikumbukwe wenye nchi si wananchi bali ni mafisadi ambao wananunua wananchi ili wapate ridhaa ya kuchukua nchi yao, kupitia vitambulisho vya wapiga kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…