Who cares

Who cares

Home tutor Dar

Senior Member
Joined
Feb 23, 2025
Posts
114
Reaction score
139
Andika juu ya anga,
chora juu ya ardhi,
piga kelele zako hadi mbinguni,
lakini ukweli hausogezwi.
Nimechoka kusubiri ruhusa,
ya kuwa mimi,
maana hata upepo hauulizi
kabla haujavuma.
Wanazungumza—
kama vile sauti zao
zinaweza kubadilisha moyo wangu,
lakini mioyo haibadilishwi
kwa maneno ya sokoni.
Andika kwenye jiwe,
andika kwenye mchanga,
andika hata kwenye historia,
lakini ukweli
utabaki palepale.
Natembea peke yangu,
si kwa sababu sina watu,
bali kwa sababu
najijua.
Wao waendelee kuandika,
waendelee kuhukumu,
mimi nitaendelea kuwa,
kwa sababu—
who cares?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom