Whitesands Hotel wanalipa sh 8,000/= (elfu nane) kwa mwezi

Kwamba wanafanya hiyo biashara ya ziada au lah haiwezi kuhalalisha kumlipa mtu elfu nane kwa mwezi, wewe ukila pale msosi ni kuanzia elfu 25 hadi elfu 40 kutegemea na menu ulochagua (kwa mtu mmoja,) yaani wewe ukila mara moja umelipa mshahara wa watu 3 hadi 5 kwa mwezi!

Uko sahihi mkuu sio kwamba nimehalalisha ila nimeeleza nachojua . Sio kwamba nakubalina nacho.
Lakini hakuna anayeweza kubisha mazingira ua uweezaji tanzania ni magumu mno. Running cost. Ile tu hali ya kutokuwa na mgoa wa umeme mwaka mzima unaweza kukuta wafanyakazi kama hao mshahara wao unaongezeka japo kwa buku 3.


Lakini hiyo ya Elfu nane naipinga . NI ujanja waajiri wengi wanatumia kuwepa malipo ya NSSF na kodi. Anaweza kupewa mshahara wa 20,000 akapewa posho fulani fulani.

Kwa mazingira ya Tanzania huwezi kuwekeza na kupata faida ukifuata sheria zote zilivyonadikwa kwenye kitabu. Ndio maana unaona wanaouja kuwekea huku ni kina RICHMOND.
 
Bado nakuna kichwa 8,000 kwa mwezi wanaishi vipi??

Kuna pool boy mmoja pale nilimtania leo nilipompeleka wifi yenu for swiming kuwa kuna kazi mshahara laki tatu kwa mwezi, akaniuliza ataweza vipi kulipa kodi ya laki tano sinza na kumudu kuendesha GX 100 yake kwa mwezi mzima.
 
Bado nakuna kichwa 8,000 kwa mwezi wanaishi vipi??



Ni kama mwanafuzi aliyemaliza chuo anakwenda field work sehemu. Ile sehemu anayofanya field wor traiing khaiwajibiki kumlipa wakimua kumlipa ni kama zawadi tu. Hawezi kushtaki sababu hata wakati anaomba alioba sehemu ya kujifunza kazi kwa vitendo.

Sasa hata hiyo 8,000 wanaweza kusema ni favour na kisheria hawana kosa lakini kiutu wote tunakubaliana sio sahihi. So wanakwenda sehemu hizo ili waboreshe CV zao au wanategea kuajiriwa.

kama kuna mtu amefanya hiyo fieldwork training kwa ziadi ya miezi miezi miwili wawasiliane na mwanasheria lakini bado nadhani itauwa vigumu kuwabana whitesand.
 
huenda mtoa sredi alikuwa na maana ya 80.000 na sio 8,000.ni typing error!
Kuna uwezekano mkubwa hiyo ikawa ni kweli, Waajiri wengi hususani hao wa Ma-hoteli hawatendi haki kabisa. Mishaala ya kisekta ilishawekwa ambayo inamtaka mwenye hoteli ndogo kulipa chini tsh 80elfu lkn haitekelezeki. Na sheria za kazi zilizopo pia hazina makali kabisa, zinamtaka Afisa Kazi kufanya ukaguzi juu ya viwango vya mishaala vinavyotolewa na endapo mwajiri akigundulika na kosa apelekwe mahakama ya Wilaya au ya Mkoa lkn huko adhabu yake aijaainishwa; hivyo mwajiri anajua kabisa akipelekwa huko watamalizana tu na hao wazee wa Suti nyeusi.Sheria nyingi zimekuwa zikipitishwa bungeni kama mchezo tu wa kuigiza, mishaala iliyowekwa ya Kisketa ni asilimia ndogo inapotekelezwa, si watu wa Hotelini hata na wanaofanya kazi kwenye Bar za kawaida, Walinzi na Ma-housegirl nao pia haki zao hazitekelezeki CHODAWU na TUPSE wamelala tu.
 
Duh! sasa noti za buku buku zilivyokuwa shida si ina maana unapewa buku kumi unaambiwa urudishe mbili?
 
Kwamba wanafanya hiyo biashara ya ziada au lah haiwezi kuhalalisha kumlipa mtu elfu nane kwa mwezi, wewe ukila pale msosi ni kuanzia elfu 25 hadi elfu 40 kutegemea na menu ulochagua (kwa mtu mmoja,) yaani wewe ukila mara moja umelipa mshahara wa watu 3 hadi 5 kwa mwezi!

Nimekusoma mwanangu!
Unachosema ni sawa, chakula tu wanachokula(breakfast+lunc or lunch+dinner) tufanye wanakula chakula cha kama 30,000 kwa siku ni sawasawa na mtu mwenye kipato cha 908,000/= kwa mwezi (NET PAY). Mtu mwenye kipato hicho cha 908,000/= akiamua kuwa anakula White Sands kila siku then mwiso wa mwezi atabaki na 8,000/=. Sidhani kama wanaonewa. Wameridhika, nd'o maana siku moja niliposahau wallet yangu yenye laki mbili (200,000/=) ambayo ni vijisenti tu kwao, niliikuta kama ilivyo kitandani na kitanda kikiwa kimetandikwa.!!!
 
Elfu nane ???? Hebu ongeza sifuri moja ili isomeke 80,000/= vinginevyo 8,000/- ni malipo ya siku.
 
Sio tu Whitesand hotel naona ni sehemu nying sana hapa Tanzania.Nenda URAFIKI TEXTILE pale Urafiki.Meneja Uzalishaji Mswahili kwa mwezi hazidi 350,000/-Mchina ambaye anafunga milango tu ya ofisi $800-1000/- kwa mwezi na watu wanaendele na kazi.
 
NAAMINI 100%
Katika harakati za kutafuta kazi nimeshawahi kukutana na mazingira hayo!
Unatumika sana tu ila unacholipwa ukikigawa kwa siku 24 za kwenda kazini unapata nauli tu ya kwenda kazini na kurudi kwa wale wanaopanda gari moja.
Imagine unalipwa 25,000/= ukikataa jamii haikuelewi eti unachagua kazi!
 
na ndio maana nikiona mtu anamsifia kikwete bungeni nachanganyikiwa
 
Jamani hivi hii ni kweli?kwa hesabu za haraka hata kama atapanda basi 1 mpaka ofisin kwenda na kurudi shs.600/=
kwa mwezi ni shs.18,000/=inawezekana vipiii hapo wadau????????????????????
 
Back
Top Bottom