which pension fund is better in Tanzania?

which pension fund is better in Tanzania?

Hamna mfuko mzuri Tanzania maana mifuko yote imekaa kisiasa, subiri kwanza wabunge watoe ule mswada wa kuchukua mafao yetu mpaka miaka 55 then ndo uje na swali lako la mifuko lakini kwa sasa hakuna mfuko mzuri
 
NSSF ndo ulokuwa mfuko unaofever customer but SSRA wamekuja sera ya kuwepo na sheria zinazofanana kwa mifuko yote mkuu
 
Afadhari PPS isingekuwa hawa SSRA kuchanganya siasa uchwara nadahani PPF wapo poa kuliko NSSF maana ilikua kwa PPF unakaa mwezi tu mmoja baada ya kuacha kazi unalamba pension yako.Vingine kama ajali kazini, sijui kufiwa, sijui kusomesha na matibabu ni mbwembwe tu maana ni terms na conditions kuzingatiwa.So uzuri wa mfuko kwangu mimi ni ule uepesi wa kuchukua ela yako pindi tu unapoacha kazi au kuachishwa kazi period
 
Kinachozungumziwa hapa ni uharaka wa kuchukua mafao yako baada ya kustaafu au ukubwa wa package ya mafao ? Kwa package pspf ndio wanatoa package kubwa zaidi.
 
Siku hizi waajiri wanapokea rushwa ktk mifuko hii ili kupeleka wanachama, Kiutaratibu kila taasisi inaomfuko ambao wanachangia kwa mgawanyo wa kiuajiri wa serikali kama serikali za mitaa ni LAPF au PSPF. Mfuko wa PSPF wanatoa pesa mingi, tatizo ni siasa!! na sera mbofu wazee wakitaka miradi ya ovyo wanalazimisha ktk mifuko hii ya jamii
 
Back
Top Bottom