When mom is alone with the kid/When dad is alone with the kid

Hahahaaa, si kweli, wababa tunacare watoto zaidi ya wamama
 
Teh...! Mtoto akiwa na baba lazima ategemee shuruba kidogo, tunawafundisha kuwa wakakamavu na kujitegemea. Mama yeye anadekeza tu, hadi watoto wakubwa. I remember since I was a little kid, nikikaa na mzee kupiga story, mifano au hadithi anazosimulia utasikia; 1. Enzi zangu nikiwa jeshini ilikuwa hivi, au 2. Nilisoma shule asubuhi ni lazima tufagie umande njiani kwenda shule au 3. Ninyi watoto wangu ni kama makinda ya njiwa (nilikuwa nafuga njiwa by that tym), yakiwa madogo wazazi wao huyalisha kwa midomo lkn yakikua huyafukuza yakatafute chakula chao menyewe ... nk .Mzee alinijenga sana kwa ushauri wa kigumu na mama yeye ni kututia moyo. Wote ni wa muhimu sana. Mungu awabariki wazazi wote...!
 
Hahaha wababa mmetuonea sana.
Hiyo ya mwisho kulia ni hatari aisee..
 
Tena ukute wanapenda hizo sulubu kibinti changu kinapigana mito na baba ake lakini kinafurahia icho mara wapigane makofi
 
Ha haaaaa, wa kwangu yeye anapenda arushwe juu. Akishushwa utamskia 'baba yenaaa ' ndo arushwe tena.

Wow anaongea maneno mengi? Wa kwangu anaongea mengi lakini hatufahamu mana kuchina si kichina
 
Hebu tutake radhi wababa wote uliotudhalilisha na thread yako hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…