Ndugu, mimi sielewi tatizo lako ni nini na liko wapi hasa? Nimeshaelezea kwamba Treni ya umeme au diesel haiamui spidi ya Treni bali inayoamua spidi ya Treni ni aina ya Reli unayojenga, kwa mfano kama unataka Treni ya kutembea 300 km/saa ktk Dar mpaka Mwanza inabidi ubadilishe kila kitu hata njia itakayopita siyo hii ya sasa na ndiyo maana unaona hata Kenya hiyo 120km/saa imebidi wapitishe sehemu nyingine tofauti na ile ya zamani, sasa hiyo yote inaangukia kwenye gharama za ujenzi na vile vile uendeshaji!
Na hapa cha muhimu klk vyote ni economy! Sasa nakushangaa sana wewe unayesema kwamba 120 km/saa siyo kitu, hivi unajua treni zlizoko sasa hivi zina kwenda km/saa?
Hazivuki 40 km/saa sasa kufikisha 120km/saa hiyo ni mara tatu yake ina maana treni ya mizigo inaweza kutoka Dar-Mwanza kwa masaa 8 wkt sasa hivi inahitaji zaidi ya siku nzima halafu unasema hauoni tofauti hapo?
Ndugu nchi hujengwa kwa hatua na huwezi kuvuka hatua moja kwenda nyingine, TZ haiwezi kuruka hatua na kujenga treni ya kwenda 300km/saa ktk chini ya 40 km/saa kwa sasa hilo haliwezekani, na hakuna nchi iliyowahi kufanya hivyo!
Hebu toka Ulaya na rudi hapa Duniani kwa maana naona tatizo ulilo nalo ni kama walilo nalo Waafrika wengi unataka kulinganisha Ulaya na Afrika unasahau kwamba TZ ina Uchumi wa chini ya 60 Bilion US dollars tu!