What's wrong with Dodoma?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

What's wrong with Dodoma??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sizinga, Jun 21, 2011.

 1. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,915
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Jamani dodoma kuna nini??katikati ya nchi, kama tulivyofundishwa tangu tupo skuli kwamba ndiyo makao makuu ya nji hii njema. Tuliambiwa na kuaminishwa kuwa hii ndiyo makao makuu ya nchi na wizara kibao zitajengwa huko badala ya Daslam. Ndiyo tangu kitambo hicho mpaka sasa nchi yetu imegubikwa na matatizo lukuki na tunajitadi kupambana nayo na kwa mafaniko yanayoenda kama kobe, lakini ni nani aliyetuaminisha kwamba wizara nyingi zitahamishiwa huko?mchawi ni nani hapa??

  Tunaaminishwa kila siku kwamba taifa hili ni changa na maskini, kumbe kuna watu wamejilimbikizia mimali/mipesa mingi ya kuweza kuilisha nchi ya burundi kwa zaidi ya miaka 8, can u imagine this?? sasa hii ya dodoma ni kweli au changa la macho?? Wabunge sasa hivi wapo mjengoni, hakuna hata anayethubutu kuuliza kuhusu dodoma, why??

  Ngoja ni-hit point!! Hivi inaingia akilini mawaziri, wabunge na viongozi wengine kuhamisha familia zao toka daslam kwenda kuishi dodoma?? Agenda ya kuhamisha wizara kwenda dodoma ipo miaka na miaka lakini hakuna kinachofanyika..ni siasa tu!! Ardhi ipo, climate nzuri, infrastructure bora, lakini kwanini hii kitu ni sumu hata kwa viongozi wetu kuona kwamba dodoma inakuwa replacement daslam??nani anajua siri ya hii kitu kugonga mwamba??naamini kuna wabunge/mawaziri wengine tangu wapo kindegaten walisoma hii kitu, lakini wapi, siasa bana!! Sijui kwanini kuhamia dodoma kwa viongozi wetu imekuwa 'inshu ngumu' hivyo! Miaka nenda rudi sasa imekuwa kama alfu-lela-ulela, ni mambo ya kufikirika tu!!

  Hivi inawezekana ugumu wa kuhamisha makao kwenda dodoma ni kwasababu ya starehe za daslam??inawezekana!! maraha yote ya daslamu nani aende dodoma??ndio kusema ile lunch ya Movenpick, New Africa Hotel, Kempisky na kwingineko ndiyo kusema is over??aagh hapana bana hatuwezi kuhamisha makao dodoma asilani!! Can u imagine, mbunge siku zote utamwona bungeni lakini malazi yake yapo daslam daily!! Kunani dodoma jamani??Twende kule ndio kusema ni mwisho wa kupigwa na kipupwe cha bahari nzuri ya Hindi hapa daslam?? Nikapigwe vumbi jekundu dodoma??Nikipata mafua nikatibiwe dodoma hospital??niende huko niwafate akina Matonya?? Big No.

  Hivi vitu vyote,ugumu wote hapa daslam, msongamano, ajali nyigi, joto kupanda kwa sana, mvua haba, polution, population na mengineyo ni matokeo/zao ya serikali yetu kukaa zaidi kisiasa badala ya kihalisia/kifikra/kiutendaji!! Huko mikoani hakuna kinachofanyika. Hii ni nchi gani bana??Hivi kuna ugumu gani kwa mfano balozi za Malawi, Mozambique, South Afrika,Shelisheli n.k zisiwe Mtwara na Lindi?? Balozi za Kenya, Ethipoia, Rwanda nk zisiwe Mwanza??Balozi za Congo , Zambia nk zisiwe Mbeya n.k? Kwanini??

  Hembu angalia barua za mkopo kwa wanafunzi lazima uje daslam, ukitaka visa lazima uje daslam, malipo ya wazee EAU daslam, kusafiri nje ya nchi lazima uje daslam,bidhaa flani-daslam, saloon za nywele-daslam,maombi ya chuo-daslam, maombi ya kazi daslam...jamani dodoma patakalika kweli?? Jamani Daslam sasahivi ndio Tanzania..hahaaaa!!nani anapenda kukaa bush bana??? Sasa ukiwauliza wanasiasa/viongozi hembu angalia majibu yao mepesi...''tunasubiria zijengwe ofisi kwanza''..hivi tatizo ni ardhi au fedha??cha kushangaza hata hapa Daslam kuna wizara na ofisi nyingi tu ni za kupanga.
  Serikali haijajenga ofisi zote hapa daslam. Viongozi wanamiss kweli raha za jiji.

  Ushauri wangu ni kwamba ujenzi wa kumbi za starehe uanze mara moja kabla hawajafikiria kuanzisha ujenzi wa wizara mbalimbali-zijengwe kumbi nyingi za starehe., club nyingi za usiku, migahawa ya 3, 4 na 5 star, madanguro na vinginevyo vingi, baada ya hapo nadhani wabunge wote watakuwa radhi kuhamia dodoma!! na kama hili halitekelezi basi hii kauli kwamba wizara zitahamishiwa dodoma ifutwe mara moja!!

  Tuchangie hoja...Jioni njema!!
   
Loading...