What is a Business? Biashara ni nini?

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,495
5,531
Leo nataka nichokoze mjadala mdogo sana ambao wengi wanaweza kufikiri kuwa ni mkubwa.Nataka kwa pamoja tushirikiane katika kutafuta jibu la swali hili "Biashara ni nini?"

Nianze kwa kutoa mifano ya biashara.Biashara ya kuuza,maji,karanga,etc ni biashara.Biashara ya kuzalisha bidhaa mbalimbali ni biashara pia. Je biashara ni nini?

Kwa mtazamo wangu Moyo wa Biashara una kitu kimoja kikuu nacho ni faida. Biashara lazima ilenge kutengeneza faida.Kama biashara haikupi faida basi hio sio biashara ni bihasara.Kwa kusema hivo si maanishi kwamba Biashara zote zina faida,hasha ila biashara zote lazima zilenge kupata faida.

Cha kushangaza watu wengi sana huanzisha biashara kwa lengo la kupata hasara.Yaani mtu anafungua duka lakini ukiangalia jinsi anavoweka mipango yake inakuwa ni mipango ya kupata hasara ili kama mambo yakienda vizuri basi anapata faida.Unajuaje kama kweli lengo na mipango yako ya kibiashara ni kupata hasara:
  1. Kuanzisha biashara ya mtaji mkubwa huku ukiwa na mtaji mdogo.Huku ni kupanga kupata hasara
  2. Kuanzisha biashara kwa sababu tu umeona mwingine ameianzisha bila kuwa na taarifa sahihi nako ni kupanga kupata hasara
  3. Kuanzisha biashara bila kujua wateja wako ni wa aina gani ni kupanga kupata hasara
Yapo mazingira na namna nyingi sana za kuanzisha biashara ambazo zinapelekea mtu kupata hasara badala ya faida na wengi huwa tunazitumia bila kujua kwamba tunapanga kupata hasara

Kwa faida ya wachache ambao wanaelewa nieleze kwa ufupi misingi ya kuanzisha biashara;Kabla ya kuanzisha biashara lazima utambue soko lako na namna ambavyo utaliteka.Kuteka soko kunaweza kuwa kwa moja wapo kati ya njia hizi ambazo ni kuwa na LOCATION SAHIHI,KUWA NA BIDHAA AU HUDUMA BORA,KUWA NA BEI RAFIKI,KUWA NA BUSINESS MODEL RAFIKI,KUWA NA UBUNIFU?UTOFAUTI

Sasa sitaki kueleza zaidi kuhusu haya maswala ila nawakribisheni wote ili tushirikiane katika kujadili uelewa wetu kuhusu biashara a changamoto zinazohusiana.

Karibuni
 
Mkuu nakuelewa sana nimetafuta namna ya kukufollow sipaoni nyuzi zako zinanichangamsha sana mkuu nikizisoma uwa najiona ni kwa namna gani nimefanya makosa mengi katika mambo ya kibiashara usife moyo endelea kuandika madini kuna watu yanatusaidia polepole
 
Hio No. 1 wachaga haituhusu sana,maana biz nyingi za mtaji mkubwa tumezianzisha kwa mtaji wa kuunga unga na tuko mjini maisha yanaendelea poa tu.
 
Hio No. 1 wachaga haituhusu sana,maana biz nyingi za mtaji mkubwa tumezianzisha kwa mtaji wa kuunga unga na tuko mjini maisha yanaendelea poa tu.
Mtaji hata kama ni wa kuunga unga ni mtaji.Believe me hata kama unaanza biashara ya milioni mia kwa mtaji wa 10 ila ukiwa strategic unatoboa mfano,mali kauli,bidii na kujituma ila ni lazima uwe umejipanga from the start.
 
Mkuu nakuelewa sana nimetafuta namna ya kukufollow sipaoni nyuzi zako zinanichangamsha sana mkuu nikizisoma uwa najiona ni kwa namna gani nimefanya makosa mengi katika mambo ya kibiashara usife moyo endelea kuandika madini kuna watu yanatusaidia polepole
Mkuu,hata mimi pia yananisaidia,Thanks for the love.Nimeamua kufanya JF kuwa shajara yangu ili hata kama nikifa basi maisha yangu yanawez kuwa baraka kwa mwengine as long as JF ipo.Kila la heri kwako
 
Back
Top Bottom