Wewe unawaza nini?

Background Check

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2019
Posts
378
Reaction score
578
Nawaza kile kinachoitwa mwisho wa dunia, au wengine wanaita kiama siku kikitokea halafu tukakuta hakuna adhabu yoyote sijui itakuwaje.

Nawaza maisha ya wanaoishi ni kutamani kuishi milele, vipi kama ukifa ni furaha na siyo adhabu kama tunavyoamini tulio wengi?

Nawaza inawezekana maisha ya wafu pengine ni kutamani kuishi tena ili vile walivyovifanya kwa uchache katika maisha yao pengine wavifanye kwa wingi zaidi, au walivyofanya kwa wingi basi wasivifanye kabisa.

Nawaza siku ya kiama vitabu vinatuambia matendo yetu yote yataoneshwa na kila mmoja atashuhudia, nawaza itakuwaje yale matendo machafu gizani watu waliyoyafanya.

Nambie we unawaza kitu gani? Kinachokupa majibu mchanganyiko.


--------
Machepele Tanzania,
Kwa sasa Dae es Salaam.
August 27
 
Nawaza kwanini umewaza hivyo? Napata majibu mawili,
Huenda umeshashiba mida hii au bado una njaa hujala,nashindwa kujua lipi hasa ndio jibu sahihi.
 
Hakuna mwisho wa Dunia lakini upo mwisho wa uhai ambapo Binadamu akipoteza uhai wake ndio inakua mwisho wa safari yake ya maisha.

Dunia ipo na itaendelea kuwepo Bali mfumo wa maisha utabadirika. Miaka ya 3000 kuendelea binadamu atafanya kazi masaa 24 bila kujali uwepo wa robots.

Janga la ukosefu wa usingizi kwa baadhi ya binadamu litakua ni miongoni mwa magonjwa yasiyotibika lakini dawa za usingizi zitatumika kwa sanaaaa

MUNGU KWANZA
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…