Wewe unadhani mwaka 2020 utakuwaje?

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
Achana na utabiri wa nyota mbaramwezi, sayari nk! Lakini wewe kama mtu mwenye maono; unadhani mwaka huu utakuaje?

Kisiasa.
Kiutulivu.
Kiuchaguzi.
Kibiashara.
Kimafanikio.
Kibinafsi.
Kiroho na kadharika.

Yes, kwa upande wangu BINAFSI, kama Mungu akiendelea kunilinda nikawepo; nadhani ni mwaka wenye changamoto za kusomesha sambamba na fursa nyingi kibiashara. Kwani upo uwezekano wa pesa kuongezeka kidogo kwenye mzunguko kwa sababu ni mwaka wa uchaguzi.

KISIASA: kama mpaka mwezi October patakuwa hapajafikiwa maridhiano ya tume huru ya uchaguzi, yenye nia ya kuruhusu wengine nao wale keki ya taifa, kama taifa tutapitia kipindi kigumu sana.

Na kwa sababu upinzani wenyewe utakuwa mkali kutokana na kungwa mkono na watu wengi waliopigika, huku ccm ikitaka ichukue kila kitu, hapo ndipo mgogoro wenyewe ulipo!

KIUCHAGUZI: Naona Lissu karudi na kutikisa sana!
KIROHO: Namwomba Mwenyezi Mungu aiboreshe imani niliyonayo kwake kuliko ilvyokuwa mwaka jana.

Sijui mwenzangu unawaza nini unapoutazama mwaka huu?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
kikundi cha kigaidi cha ccm watateka na wataua sana watu zaidi ya miaka minne iliyopita na hawatachukuliwa hatua yoyote popote na yeyote.
 
Mwaka huu ccm wanaweza wakashangaa kidogo, hata kama hawatashindwa lakini hasira za watu zitaonekana baadhi ya maeneo
 
Back
Top Bottom