Wewe uko sawa?

Wewe uko sawa?

myroom320

Member
Joined
Apr 17, 2013
Posts
40
Reaction score
16
kasoro.jpg



Hujawahi kufikiria na hutaweza kuamini, lakini ukweli ndio huu. Wewe unaweza kuwa sababu kubwa sana ya mpenzi wako kuonekana ana kasoro kibao,hawezi kuwa mpenzi sahihi kwako henda ni kwasababu ya umakini ulionao na tabia yako kwake ambayo inasababisha kuzalisha ubaya kutoka kwake yani kuonekana hafai hata kidogo.

Na utakuja kushangaa mtu yuleyule ambaye alionekana mbaya kwako, mwenye mapungufu mengi, na hafai anakuja kuwa mzuri sana na kufaa pindi tu atakapooa au kuolewa na mtu mwingine atakayemthamini, muheshimu na kumtunza vizuri inavyotakikana.Kuna kazi kubwa ya kufanya unapokuwa na mwenzi wako. Ulishawahi kulifikiria hilo?

Je ni yapi utakayoweza kufanya kuuonyesha uzuri wa mwenza wako uliojificha?

 
umeongea kweli tupu hua hatujiangaliii tunakosea wapi tunachojua ni kujudge tu
 
Ni kweli kabisa ukiona mtu anamtoa sana kasoro mwengine inabidi ajichunguze kwasababu tatizo linaanza kwake yeye mwenyewe....Ukiona mtu anapenda sana kuhukumu wengine ujue hajiamini!!
 
Basi wanaume wengi wa jf watakua na matatizo ya kutojiamini ndio maana kutwa kulalamika mwanamke hivi, mwanamke vile lakini mwisho wa siku wanawake haohao wanaendelea vizuri kwa wengine.
 
Basi wanaume wengi wa jf watakua na matatizo ya kutojiamini ndio maana kutwa kulalamika mwanamke hivi, mwanamke vile lakini mwisho wa siku wanawake haohao wanaendelea vizuri kwa wengine.
🙂 🙂 🙂 🙂 🙂 🙂
 
Back
Top Bottom