Mara nyingi nimejiuliza sana, hasa kwa watu wanaomwamini MUNGU aliyeziumba mbingu na nchi. Ni kwanini kuna ahadi nyingi sana za kiMungu katika maandiko yake lakini uhalisia katika Maisha ya watu sio kile kilicho kwenye maandiko , leo hii watu ni wagonjwa sana na kila mtu anaugulia matatizo yake na ni siri na mungu wake, watu wana umaskini wa kutosha tu, mishahara inaishia kwenye matumizi ya kawaida na hakuna kiasi cha ziada kuwapa wahitaji au kufanya maendeleo,wakulima wanalima lakini hakuna ziada. Hivyo kila mmoja anafikiria kuiba au kupiga dili hatakama ni kuiba au kudhuru wengine, mwajiriwa anawza kumwibia mwajiri wakati mwajiri anamkamua mwajiri kisawasawa ili kupata faida zaidi. Kwa jumla fikra zetu ni kuiba tu ubunifu na mawazo mapya hakuna.
Mifumo ya kiutawala ni shida tupu, siasa inakula roho za watu kana kwamba waliwaumba wao, wanadamu wanauadui miongoni mwao hatakumchinga mwanadamu mwingine, tumeona yanayofanywa na Boko haram, ISIS,Alkaida nk, hakuna woga wala hofu ya kuuwa ni kawaida tu sawa na kukata majani shambani, je ujasiri huu unatoka wapi?.
Binadamu hafanyi ziada kumwokoa/kumsaidia mwingine bila pesa, ukienda hospitali, mahakamani, ofsini kwa Mtu na nk, kinachoangaliwa na mfuko wako, hizo ndizo fikra zilizojengwa miongoni mwetu, hakuna kubuni vitu vipya, watu wamepumbaa na mambo manyonge na ya zamani, akili zetu pia zimekuwa za zamani hivyohivyo.
Je ndivyo MUNGU alivyopanga iwe? Ukisoma kitabu cha mwanzo 1:26 Mungu anamfanya mwanadumu kwa mfano wake, anambariki na kumwamuru kuzaa, kutawala na kutiisha uumbaji ambao MUNGU amempa hiyo ni mwanzo 1.28. Tafakari kidogo!!! Uumbaji wote Mungu amemkabidhi mwanadamu autunze, umletee Maisha bora na awe na amri juu ya kila kitu alichokiumba, na pia amembariki kwa maana nyingine amempa nyenzo na mbinu zote za kumuwezesha kuishi vyema kwenye mazingira hayo.
Tafakari tena!!!, je ndivyo ulivyo wewe, unamiliki? Unatawala?, umezaa nini kuwaonyesha wangine kuwa huu ndiyo uzao wako? Neno kuzaa halishia kwenye watoto ni zaidi ya kuumba vitu vipya vinyokutofautisha na wengine, (qualities of creating things)
Nikurudishe nyuma kidogo hapo mwanzo 1.26, wakati MUNGU anamfanya mtu kwa mfano wake, ni roho ndiyo iliyoumbwa hivyo mtu aliyepewa kutawala ni roho, na mtu aliye umbwa kwa mfano wa Mungu ni roho siyo mwili, mwili wako ni mfano wa baba yako na Mama yako na hauna dili lolote na MUNGU isipokuwa ni nyenzo ya kukusaidia kutimiza kusudi la Kuzaa, kutawala na kumiliki. Shika sana hili litakusaidia sana kupangua mambo mengi ya mwili yanayokwaza mafanikio yako ili ufanikiwe.
Nikumegee kidogo tu hapa kwa ajili ya ufahamu . mwili ni kama gari linakusaidia kutekeleza majukumu yako ya kazi, mfano gari likaharibika unaacha majukumu yako?, mfano unasafiri kwenda morogoro gari likaharibika chalinze jee unaishia hapo? Bilashaka utashuka na kupanda lingine na Moro utafika na kufanya kilichokupeleka. Kamwe usiruhusu mwili ukuzuiwe kumiliki , kuzaa na kutawala hauna chake wenyewe ni gari tuu, roho ndiyo wewe na ndiyo iliyo pewa kumiliki,kuzaa na kutawala.
Nilikuwa najenga Msingi ilihoja iingie vizuri kwenye fikra zetu, kwa mujibu wa MUNGU mwili na nafsi zinanaletwa kuungana na roho katika mwanzo 2:7, yaani nafsi na roho zinatoka kwa MUNGU wakati mwili unatoka kwenye udongo na vinaungana kukufanya wewe. Na ndiyo maana mwili unapinga chochote kutoka kwa MUNGU usipoutendea kwa akili, nasisitiza tena usiusikilize mwili haunampango wa kukufanya ufanikiwa kwa lolote katika utawala wa huu hapa dunia kwa mfumowa ki MUNGU. vinginevyo ubakie tu kupiga dili na kama huna sehemu za kupiga dili ukubali kubaki masikini milele.