Matanga
JF-Expert Member
- Nov 13, 2019
- 2,281
- 3,988
ULICHONACHO KINA THAMANI KUBWA SANA
Wenye Chakula hawana appetite (hamu ya kula) na wenye appetite hawana chakula. Wenye majumba ya kifahari wanakosa usingizi, na wenye usingizi wa kutosha hawana hata pakulala. Wagonjwa mahututi wanaomba uzima, wazima wa afya wanajiua. Wagumba wanalilia watoto, wasio wagumba wanatoa mimba na kutupa watoto chooni. Wenye mialiko mingi hawana nafasi ya kwenda na wenye nafasi hawana mialiko.
Wasio na kope wamejikubali kama walivyo, wenye kope wanavaa za bandia. Anayepewa upendo hauthamini asiyependwa analilia upendo.
Wenye amani wanaomba vita na kutishia machafuko, wenye vita wanalilia amani.
Mwenye nafasi ya kusoma na ada analipiwa hataki shule wala haitilii maanani, mwenye kiu ya kusoma hana ada.
Ni kama binadamu hajui anachokitaka hivyo hata akipata alichodhani anataka bado haridhiki kwani sicho hicho anachotafuta.
CHA KUSHANGAZA
1. Hicho unachokidharau Leo ndicho kilikuwa kinakuliza jana na kukunyima usingizi.
2. Hayo unayotafuta Leo pia kesho hayatakuwa na mashiko kwako.
MAISHA NI FUMBO LILILOSHEHENI VIFUMBO KAMA MFALME SULEIMAN ALIVYOSEMA " TUNAFUKUZA UPEPO" ambao hatutakaa tuukamate!!
SHUKURU KWA UHAI. VINGINE VYOTE VINATHAMANI USIPOKUWA NAVYO, UKIVIPATA THAMANI YAKE INAISHIA HAPO. HIVYO USIRUHUSU VIKAKUTAWALA,UKIZINGATIA HIVYO UTAISHI KWA AMANI BILA KUUTESA MOYO WAKO.