Wewe ni siri

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
10,569
Reaction score
21,075
Tunza siri zako mwamba!


___________________

1. Siri ni maisha wewe! Huna siri, huna maisha!
2. Ukiweza kujificha adui asikuone lakini wewe ukawa unamuona jua ushindi ni wako hata kama unasilaha dhaifu.
3. Kujificha ni moja ya kanuni za ushindi! Kitu kinachofichwa huitwa siri. Wengi wameshindwa kuficha siri zao!
4. Wakipata jambo wanawashwa, wakilisema muwasho unaisha.
5. Wakipata safari wanaagaaga kwa kila mtu hadi safari inaahirishwa.
6. Sikiliza! Watu wakijua siri za mafanikio yako watakutoboa macho usione mafanikio yako kama Samson.
7. Samson alitobolewa macho baada ya kushare siri zake na Pisi yake Delila.
9. Hata mwanamke anayelala kifuani kwako asijue siri zako* (Mika 7:5-6). Unaona mambo hayo?
10. Yusufu aliuzwa na ndugu zake kwa sababu ya kusema ndoto zake hovyo.
11. Sasa na wewe washirikishe ndugu zako siri zako wakakuuze😄😀
12. Huwezi kuwa Tajiri Mkubwa kama huna siri, huwezi kuwa Nabii Mkubwa kama huna siri!
13. Siri ni tafsiri ya ushindi. Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo (Mithali 25:2).
14. Siri ni ulinzi. Mtu asiye na siri hana ulinzi. Siri ipo kwa ajili ya mafanikio.
15. Ili ufanikiwe lazima ujue siri fulani fulani. Na ukiishazijua ficha! Waliofanikiwa wanafanya hivyo.
16. Yaani utashangaa tu ana nyumba kila mkoa, utashangaa tu ana magari ya biashara gari huwa hawatangazi.
17. Wanatumia nguvu kubwa kuhakikisha siri zinabaki kuwa siri.
18. Ukiwauliza watakwambia, jitume, fanya kazi kwa bidii, amka mapema!
19. Uamke mapema kwenda wapi? Hawakwambiii😄😄.
20. Na wewe jifunze kuficha siri zako! Habari za mficha uchi hazai ni tungo za wahuni wa kale! We ficha tu😄😄
21. Kama una mpango wa kufuga kuku usiwaambie watu, anza kimyakimya washitukie una kuku. Ukianza kutangaza hutofuga.
22. Ukifuatilia utakuta familia nyingi zilizochoka hazina siri! Mama anamwaga siri za baba kwa watoto, baba anamwaga siri baa!
23. Unakutana na mtu leo humjui, unampa hadi siri zako za ndani. Huu ni wehu!
24. Ukiona chimbo sehemu piga kimya kimya kama siafu, siafu utamkuta ndani ya nguo mbali kabisa anakung'ata. Alifikaje huko? Hujui😄.
25. Mbu huwa anakosa madili mengi kwa sababu ya yabia yake kupiga kelele anapoona damu. Mbu ni kama wewe sasa!
26. Bila kutunza siri kila kitu kitakuwa kigumu kwako. Hata mapenzi yatakuwa magumu.
27. Unapata dili unatoka juu juu kama nyama dukani kuwatangazia watu. Utasubiri sana.
28. Usiwaonyeshe watu ng’ombe anayekupa maziwa,watampa sumu ukose maziwa.
29. Ficha mipango yako; fichua matokeo. Fanya kama mimba vile. Inavyotengenezwa hatuoni, tunaona matokeo tu😄😄.
29. Coca cola ingetoa siri zake isingekuwa namba moja kimauzo duniani.
30. Man is not what he thinks he is, man is what he hides ," alisema André Malraux.
31. Wazungu wameunda mpaka jamii za siri. Wanaziita Secret Society. Hawa ndo wanatawala dunia.
32. Hawaruhusu hata watoto wao kuoana na watu wa kawaida.Wanawachagulia watoto wao wachumba.
33. Sisi tukifanya hivyo tunaambiwa ni ushamba. Matokeo yake watoto wetu wanaingia kwenye ndoa na mijitu ya hovyo.
34. Watoto wetu wasipoolewa na majitu ya hovyo, basi wanaoa majitu ya hovyo na kuzaa majitu hovyo😄!
35. Mafanikio ni mchezo wa kuangushana, ukiweza kutunza siri huwezi kuangushwa.
36. Kama Mungu mwenyewe mambo yake ya thamani ameyafanya siri, wewe ni nani hadi utangaze mambo yako?
37. Kwani nani alimuona Mungu? Mungu angekuwa anazubaa zubaa kuna watu wangemuwinda wamuue😄😄
38. Herode alishindwa kumuua Yesu kwa sababu wazazi wake walifanya siri.
39. Mjukuu wangu ukipata mimba unapiga picha tumbo unashare. Huyo mtoto unamuweka hatarini.
40. Usijitenge na watu lakini watenganishe watu na siri zako.
41. Usiri ni hatua muhimu sana kuelekea kwenye mafanikio. Ukianza kutunza siri zako mambo mengi yatakaa kwenye mstari.
42. Utajiri hupenda watu wenye tabia ya kujificha. Utajiri unahitaji usiri; umasikini unahitaji kujianika.
43. Matajiri wanaficha utajiri kwa kuishi kimaskini, maskini anaficha umaskini kwa kuishi kitajiri!
44. Mipango ya mafanikio ni kama nguo ya ndani, ni muhimu kuivaa lakini si muhimu kumuonyesha kila mtu kwamba umeivaa!
45. Hapa umetupiga ndoige wote tusioweza kutunza siri🤣🤣🤣.
 
nimeipenda sana hii umebariki siku yangu
 
No reform no election.

Tafuta Hela Ndugu hizo methali utazisahau zote.
 
Hii aione@pesa. Kila kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…