Wewe nani mpaka umridhishe kila mtu?

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Ni ngumu sana kustahimili maumivu hasa pale unapoumizwa na mtu uliemtarajia kukupa furaha.Hakuna budi zaidi ya kuvumilia tu kwasababu kuendelea kufuga maumivu ni kujisababishia maumivu zaidi.Duniani hakuna furaha ya kudumu wala raha ya kudumu.

Ukiwa mpole utachokozwa ili useme.Ukiwa mkarimu utatukanwa na kurogwa eti unajifanya una pesa.Ukiwa msikivu utaitwa mwenye kibri.Ukiwa upo bize na mambo yako utaambiwa hujumuiki na watu.Hakuna jema ambalo binaadamu ukifanya kwa binaadamu wenzako litakuwa na maana.

Kuumbwa kwetu kuna kusudi kubwa sana na kusudi lenyewe ni kufanya yalio sahihi na si kuridhisha watu.Kama Mungu anafanya kila kitu kwetu na bado anatukanwa wewe unafanya kipi kikubwa kumshinda Mungu ili usitukanwe!. Muhimu katika hii dunia ni kufanya yalio sahihi haijalishi yatachukiwa na wengine au yataungwa na wengine wewe fanya tu.

Anachokiridhia Mungu hata watu wakikichukia ni sawa na bure tu.Maisha yetu yapo ndani ya muda maalum hivyo ni lazima utende mambo maalum kabla haijakufika siku maalum itakayokutenganisha na vipenzi vyako.

CHUNGA SANA

Amini usahihi katika maisha yako kuliko kuridhisha watu.
 
Back
Top Bottom