Elections 2010 Werevu wameruhusu wapumbavu kujiamini!

Mkulima mimi

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
233
31
KATIKA Ulimwengu wao, magwiji wa hisabati, falsafa, historia na wanaharakati wa haki za binadamu hawathubutu kupuuza rekodi ya mwenzao, Bertrand Russell.
Russel alipata kutangazwa kuwa ni mwanafalsafsa wa karne ya 20. Kati ya matokeo ya harakati zake ni pamoja na kuwahi kuwa mfungwa wa kivita.

Marehemu Russel ni raia wa Uingereza aliyezaliwa Mei 18, mwaka 1872, ambaye uliokuwa utawala wa Adolf Hitler unatambua misukosuko yake yenye nguvu za kimantiki.

Ni miongoni mwa watu waliotoa mchango mkubwa wa mabadiliko duniani, akijipambanua kama mwanaharakati mpinga vita, mwanahisabati, mwanahistoria na mwanafalsafa; hasa falsafa ya lugha.
Enzi za maisha yake, kabla ya kifo chake Februari 2, mwaka 1970, akiwa na umri wa miaka 97, aliongoza harakati za kupigania biashara huru (free trade).

Kwa upande mwingine, enzi zake Russell alikuwa mpinzani mkubwa wa taratibu na sheria za kimwinyi au kwa lugha nyingine za kibeberu (imperialism).
Marekani wanamtambua kama mmoja wa wanafalsafa vigogo waliopinga mpango wa taifa hilo kuishughulikia kivita Vietnam.

Mwaka 1950, Russell alitunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel kutokana na juhudi zake, hasa maandishi yake yaliyokuwa yakiibua mbinu na fikra za kupigania na kutetea utu na uhuru wa mawazo.
Kwa kuzingatia muhtasari wa maelezo haya, ni dhahiri kuwa Russell enzi zake aliifahamu dunia na wanadamu. Alifahamu hila, ubaradhuli, werevu na upumbavu wa viongozi wakubwa na maarufu duniani.

Si makosa makubwa kukiri aliitambua dunia na dunia ilimtambua. Aliwatambua walimwengu na ulimwengu ulimtambua. Kwa hiyo, alikuwa na mamlaka ya kimantiki kuizungumzia dunia na watu.
Kwa kutambua hivyo aliweka bayana maoni yake kuhusu dunia. Akasema harakati zake ki-dunia zilimruhusu kuwagawa watu katika maeneo mawili.

Eneo moja ni watu werevu. Eneo jingine ni la watu aliowaita wapumbavu, mabaradhuli au mazuzu. Kwa kuzingatia makundi haya ya watu, akabainisha tatizo la dunia.........


Endelea kusoma hapa:

Werevu wameruhusu wapumbavu kujiamini


Source: Raia Mwema
 
Back
Top Bottom